AMANI YA KRISTO NA AMANI YA ULIMWENGU

Kuna makundi mawili ya Amani, nayo ni:-
(1) Amani inayokana na ulimwengu
(2) Amani inayotokana na KRISTO =hii ndio Amani ya Kristo.
YOHANA 14:27 = Amani nawaachieni, amani yangu nawapa, niwapavyo mimi sivyo ulimwengu utoavyo.
Ukiangalia kwa makini katika mstari huu utagundua kwamba Yesu anatoa Amani, na Ulimwengu nao unatoa Amani,
lakini Amani hizi ni tofauti kabisa,. . . . Atupavyo Yesu sivyo kama ulimwengu utoavyo,. . . Maana yake ni kwamba, Amani aitoayo Yesu . Siyo kama Amani inayotolewa na ulimwengu.

IFUATAYO NI TOFAUTI YA MAKUNDI HAYA MAWILI YA AMANI
Tuanze kuizungumzia AMANI INAYOTOKANA NA ULIMWENGU
kuna aina mbili za Amani zinazotokana na ulimwengu
(a) Amani ya kibinaadamu iliyo sawa na njia za ulimwengu,
(b) Amani shetani mkuu wa ulimwengu.
¤ AMANI YA KIBINAADAMU ILIYO SAWA NA NJIA ZA ULIMWENGU
=Biblia inatuambia kwamba, hatupaswi kuifuata Amani ya namna hii ya kibinaadamu,
TORATI 23:6, Usifuate Amani yao, wala heri ya siku zako zote, milele,
Amani ya kibinaadamu, ni amani anayokuwanayo mtu kutokana na kupenda kitu anachochagua kukifanya kutoka na njia za kawaida za ulimwengu
Mtu yeyote anaweza kuwanayo Amani hii inayotokana na ulimwengu hata kama haja Okoka
Mfano‬
=Mtu amekaa muda mlefu bila kazi, na akaletewa taarifa ya nafasi ya kazi mahari furani, Mtu yeyote katika mazingira haya ni lazima atakuwa ni mwenye Amani, na kwenda haraka kwenye kazi hiyo. .Hii ni Amani ya kawaida ya kila mtu wa ulimwengu.

=Mtu aliyekosa kitu furani kwa muda mlefu, siku akija kukipata kitu hicho, nilazima atakuwa ni mwenye Amani,
=Mtu akipata mchumba anayempenda pasipo kulazimishwa na wazazi, ni lazima atakuwa ni mwenye Amani,
=Mtu akipata kazi yenye mshara alioutarajia, ni lazima atakuwa ni mwenye Amani,
=Wanandoa waliotafuta mtoto kwa muda mlefu, siku wakipata mtoto ni lazima watakuwa ni wenye Amani
=Mtu akipona ugonjwa uliomsumbua kwa miaka mingi, ni lazima atakuwa ni mwenye Amani.
Hizi zote ni amani za kawaida za kibinaadamu zitokanazo na ulimwengu huu.
MUNGU AKUBARIKI. ‪‎BY_MWINJILISTI‬ Gerard Robert

Comments