Aponywa ugonjwa mbaya uliosumbua utumbo wake baada ya maombezi.



Mungu anafungua watu hata sasa.

"Hapo kabla nilikuwa sioni umuhimu wa kwenda kanisani,niliweza kukaa hata mwaka mzima bila kwenda kanisani,sikuona umuhimu wa kusali wala kuwa karibu na Mungu.. nilichojali ni raha za dunia hii... Mwaka jana nilianza kuumwa, niliteseka sana..hadi siku moja nikawa nawaambia familia yangu kwamba natafuta mchungaji wa kuniombea kwa maana roho yangu inaamini Mungu ndiye jibu la matatizo yangu,lakini familia iliniambia niende tu kwenye kanisa lolote lililo karibu ili nikaombewe,nilikataa.. Nikawaambia mimi nataka kuombewa na mchungaji aliyesimama kwenye wokovu kwelikweli!

Siku hiyo hiyo baada ya masaa kadhaa,alikuja kijana flani pale nyumbani,na wakati wa mazungumzo.. aliniambia niende kwenye nyumba ya ufufuo na uzima, pale kuna Mungu wa kweli na utapona kwa jina la Yesu.. Sikupoteza muda,nilienda na kuonana na mmoja wa wachungaji wa pale,aliniombea..ilikuwa nifanyiwe operation kubwa kwenye utumbo mkubwa wa chakula kutokana na ugonjwa ulipo lakini Mungu alimuonyesha huyo pastor kwamba hiyo operation haikuwa nzuri kwangu kwahiyo nikaombewa ili Yesu aitengue hiyo operation isifanyike... na kwa uwezo wa Mungu hiyo operation kweli sikufanyiwa tena! Hadi leo hii mimi ni wa nyumba ya ufufuo na uzima,nimepona..Siku zote nitamshukuru Mungu kwa kunichagua,kuniponya na kunifanya niwe mmoja wa watoto wake. Amen"

MUNGU KWETU NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE

Comments