''BAADHI YA MBINU ZA KUDHIBITI MOYO WAKO NI:- (Kipengele cha 2 hadi cha 6.)

na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira


ii) ANDAA NA TAYARISHA MOYO WAKO KABLA YA KULALA.
Kabla ya kwenda kulala, na kwa msaada wa ROHO MTAKATIFU kagua Moyo wako kwa kupitia Shughuli na Ratiba Nzima ya Maisha yako katika siku hiyo, ili Uweze kutubu kabla ya Kulala. Biblia inatuasa TUTAFAKARI Vitandani Mwetu na Kutoa Dhabihu za Haki (Zaburi 4:4). Moyo una Matatizo na ni Mdanganyifu kuliko Vitu vyote. Kabla ya mtu kuwa mgonjwa moyo wake huugua kwanza. Ndani ya Moyo wa Mtu ndipo zilipo Chemchem za Baraka (Uzima) au laana (mauti) alizopewa na YESU siku ya Uumbaji wake; na Amepewa kuchagua anachotaka (Yeremia 17:9). Hata kama umekwisha kuomba na Mwenzako lazima wewe Mwenyewe utafakari yale yote Uliyoyatenda kwa kuwa Ratiba nzima ya mapito na Mwenendo wako iko kwenye Moyo wako mwenyewe.

(''Neno hili lenye HEKIMA na UFAHAMU Kuhusu Baadhi ya Mbinu za Kudhibiti Moyo wako Juu yako Mwana wa MUNGU lina Vipengele 9, Usikose, Usipitwe na hata kipengele kimoja, Soma kwa HEKIMA NA UFAHAMU, Omba ROHO MTAKATIFU ILI UWEZE KUTOKA Mwana wa MUNGU, Husiwe tena wa Zamani, Husiwe tena chini ya Utumwa wa Shetani,... BWANA YESU Awe nawe


 iii) KUJAZA NENO LA MUNGU KWA WINGI MOYONI MWAKO NA KULITAFAKARI.
Ili USIJE KUGOMBANA na MUNGU Hakikisha Unalijaza NENO la MUNGU kwa Wingi Moyoni mwako. Neno linasema “Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako nisije Nikakutenda dhambi” (Zaburi 119:11). Ukiliweka Neno LAKE kwa wingi Moyoni mwako, Maudhi hayatakusumbua. Usipojaza Moyo wako na NENO la MUNGU, basi Adui zako Watakupata kwa Maneno yao. Hakikisha Maneno yako YANAAMBATANA na jinsi MUNGU ANAVYOSEMA. Umba Tabia ya KUTAFAKARI NENO Moyoni mwako kwa Wingi na USIACHE Kuelezea habari za TUMAINI Lako kwa Wengine.''

(''Neno hili lenye HEKIMA na UFAHAMU Kuhusu Baadhi ya Mbinu za Kudhibiti Moyo wako Juu yako Mwana wa MUNGU lina Vipengele 9, Usikose, Usipitwe na hata kipengele kimoja, Soma kwa HEKIMA NA UFAHAMU, Omba ROHO MTAKATIFU ILI UWEZE KUTOKA Mwana wa MUNGU, Husiwe tena wa Zamani, Husiwe tena chini ya Utumwa wa Shetani,... BWANA YESU Awe nawe.'')


 iv) TAFUTA YA MUNGU KWANZA.
MUNGU ANATAKA UMPENDE KWANZA na kitu chochote KISIKUTOE katika kumpa MUNGU Nafasi ya KWANZA. MUNGU Anataka TUTAFUTE ya JUU, lakini sisi bado tunafanya kama Dunia inavyofanya kwa kuyangalia Mazingira yetu, Badala ya kuangalia AHADI ZA MUNGU Amesema nini Juu yetu.

-Mfano: MUNGU AMEAHIDI Atanipa vya SIRINI, kazi yangu ni KUKIRI hivyo hadi IMEKUWA, badala ya Kuangalia hali inayonizunguka. Ndipo Anasisitiza kuwa TUJISHUGHULISHE na Mambo yake, Naye ATAJISHUGHULISHA na Yetu. “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na KRISTO, Yatafuteni yaliyo Juu, KRISTO Aliko, Ameketi mkono wa Kuume wa MUNGU. Yatafakarini yaliyo Juu, siyo yaliyo katika Nchi.” (Wakolosai 3:1)''

(''Neno hili lenye HEKIMA na UFAHAMU Kuhusu Baadhi ya Mbinu za Kudhibiti Moyo wako Juu yako Mwana wa MUNGU lina Vipengele 9, Usikose, Usipitwe na hata kipengele kimoja, Soma kwa HEKIMA NA UFAHAMU, Omba ROHO MTAKATIFU ILI UWEZE KUTOKA Mwana wa MUNGU, Usiwe tena wa Zamani, Usiwe tena chini ya Utumwa wa Shetani,... BWANA YESU Awe nawe.'')

 v) UTII KWA NENO LA MUNGU
Hali yako ya KUTII NENO LA MUNGU ndiyo inayoonyesha UKO UPANDE WA MUNGU au wa Dunia. Ukikubali kujitiisha wakati unapoelezwa jambo la kujikosoa ili ubadilike, basi utakuwa mwenye Hekima na Akili Kweli. Katika Biblia tunasoma, “Amini, amini, nawaambia, saa inakuja na sasa ipo, wafu watakaposikia sauti ya mwana wa MUNGU, na wa wale wasikiao watakuwa hai” (Yohana 5:25)

- Mfano: Ukichunguza, utabaini kuwa wanawake wengi hawana shida ya kupenda waume zao, bali wanashida katika kutii. Ni vyema kujua kuwa asipojitiisha chini ya mumewe hata kama Ananena kwa lugha kiasi gani ajue Hukumu inamsubiri. Vivyo hivyo wanaume wameagizwa kuwapenda wake zao na kukaa nao kwa akili kama viumbe dhaifu. Wewe mume usipotii agizo hili, la kumpenda mke wako, jiandae kwa hukumu ya milele.

- Mfano: MUNGU ameagiza kila mtu amtolee sehemu ya kumi ya mapato yake, lakini wengine hawataki kutii amri hii. Ukweli ni kuwa kila asiyetoa fungu la kumi anamwibia MUNGU Mwenyewe na adhabu yake ataiona akiwa hai na hata baada ya kufa. MUNGU hahitaji fedha ya mtu, bali anaangalia kama mtu anafahamu kuwa YEYE ndiye Asili ya yote aliyo nayo.

(''Neno hili lenye HEKIMA na UFAHAMU Kuhusu Baadhi ya Mbinu za Kudhibiti Moyo wako Juu yako Mwana wa MUNGU lina Vipengele 9, Usikose, Usipitwe na hata kipengele kimoja, Soma kwa HEKIMA NA UFAHAMU, Omba ROHO MTAKATIFU ILI UWEZE KUTOKA Mwana wa MUNGU, Usiwe tena wa Zamani, Usiwe tena chini ya Utumwa wa Shetani,... BWANA YESU Awe nawe.'')

 vi) LINDA SANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE
Ili uwe mtu wa MUNGU inakubidi ULINDE sana Moyo wako kuliko vyote Unavyolinda, Ukiangalia sana KUENENDA na KUTENDA kwako. MUNGU huwa Anaruhusu upite katika Mapito Fulani ili Ufikie mahali pa kuwa kama Anavyotaka. ANATAKA kuondoa Moyo wa JIWE ndani yako na Kuweka Moyo wa NYAMA. MUNGU Analeta MOYO Mpya na ROHO Mpya ndani yetu ili tushike MAAGIZO na SHERIA zake, ndipo tunakuwa WATU WAKE Kwelikweli. Kama tusomavyo kutoka kitabu cha Ezekieli kuwa “Ndipo akaniambia, “maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba na kuingia katika bahari; maji yatokezwayo kuingia baharini, na maji yake yataponyeka” (Ezekieli 47:8). Upande wa Mashariki wa Mwili wa Mtu ndiko Moyo wake ulipo na Maji yatatoka Patakatifu pa MUNGU, Yakitafuta Moyo wa Mtu na Akikutwa yuko Tayari KUBADILISHWA ATABADILISHWA, kama tulivyoona katika Sura iliyopita, Mwanadamu ana sehemu Tatu, Mwili, Nafsi na Roho na kilicho na Usumbufu kuliko vyote ni Nafsi, Ambayo inasababisha Mwili au Roho kuadhibiwa. Maji yakija na kuingia Moyoni, yakifuata ile ChemChem iliyo ndani ya Moyo, na Ikikutwa ina matope inaachwa kama ilivyo. Matope hapa ni ule uovu uliotajwa huko nyuma."

(''Neno hili lenye HEKIMA na UFAHAMU Kuhusu Baadhi ya Mbinu za Kudhibiti Moyo wako Juu yako Mwana wa MUNGU lina Vipengele 9, Usikose, Usipitwe na hata kipengele kimoja, Soma kwa HEKIMA NA UFAHAMU, Omba ROHO MTAKATIFU ILI UWEZE KUTOKA Mwana wa MUNGU, Usiwe tena wa Zamani, Usiwe tena chini ya Utumwa wa Shetani,... BWANA YESU Awe nawe.'')

Comments