''BAADHI YA MBINU ZA KUDHIBITI MOYO WAKO NI:- (Kipengele cha saba hadi cha mwisho)

 Na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira


vii) ENENDA KATIKA ROHO ILI KUMSHINDA IBILISI.
Mkuu wa anga ndiye aliye na funguo za Kusababisha Watu kufanya Dhambi kwa sababu dunia yote inaonekana kuwa imewekwa chini ya hasira yake. Ibilisi amepewa Wote WATEMBEAO katika MWILI ambapo Anawaburuza bila kujali hali yao. Kwa hiyo mtu AKIENENDA katika ROHO Ibilisi HANA NAFASI ya KUMPATA. Tunasoma katika Biblia; “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mlizitenda zamani kwa kufuata kawaida ya Ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uweza wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine” (Efeso 2:1-3).

Kama unatembea katika Ujinga utapata Viboko ambavyo ni majaribu, hadi hapo utakapotambua unatakiwa UTOKE katika hali Uliyonayo. Neno linasema, “Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, Alituhuisha pamoja na Kristo; yaani tumeokolewa kwa Neema” (Efeso 2:5).

viii) UUVUE MOYO WA ZAMANI
UTU WA KALE unakaa kwenye Moyo (Efeso 4:17-30). UJINGA nao siku zote unakaa Moyoni na HUONDOLEWA kwa Fimbo ambayo ni Majaribu. Ukiona Majaribu yanakujia katika SHUGHULI na MAMBO yako Ujue UNAFUNDISHWA ili UTOKE katika huo UJINGA, kwa KUVUA MOYO WA ZAMANI na KUINGIZA MOYO MPYA. Tunasoma katika Biblia kuwa, “Basi nasema Neno hili, tena nashuhudia katika BWANA: tangu sasa Msienende kama mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao ambao Akili zao zimetiwa Giza, nao Wamefarikishwa na UZIMA wa MUNGU, kwa sababu ya UJINGA Uliomo ndani yao, KWA SABABU YA UGUMU WA MIOYO YAO;” (Efeso 4:17-18).

ix) JENGA TABIA YA KUWAPENDA WANAOKUZUNGUKA.
Jamii inayokuzunguka ina Mahitaji mengi na Hulka tofauti. Watu hawa wamegawanyika katika MAKUNDI Mawili Makubwa ambayo ni MAADUI na WANAOUDHI:-
a) MAADUI:-
Hawa Wanayo tabia ya KUTOKUPENDA WEWE UFANIKIWE. Kwa kuwa Biblia imesema Adui yako UTAMSHINDA KWA UPENDO, basi Vita iliyopo kati yako na Adui yako UTAISHINDA tu pale Utakapopigana huku Ukiwa na UPENDO na FURAHA. MAANA ya Kumpenda Adui SIYO KUJIPELEKA KWAKE AKUMALIZE, Bali USIMWEKEE CHUKI Moyoni Mwako. Mtendee Mema Adui yako badala ya KURUDISHA Ubaya kwa Ubaya.

Ukitaka KUWASHINDA Adui zako MTAZAME na KUMTEGEMEA MUNGU Kama Mfalme Yehoshefati alivyofanya. Mfano:- Ukimwona ana Shida na Wewe una UWEZO wa KUMSAIDIA, USIACHE kwa Alikutenda vibaya. Ukiona kitu chake kinaharibika na Wewe unaweza KUOKOA Usiache kwa kuwa ni Adui bali OKOA, na kwa Namna hiyo Utampalia MAKAA Kichwani pake naye ATAPIGWA SANA na MUNGU kwa MAKOSA YAKE. Mara nyingi Wabaya wetu HAWAADHIBIWI kwa kuwa TUNAMWINGILIA MUNGU kwa Kuanza KUENDESHA SHAURI na KULIPA KISASI. Tunataka KULIPA Kisasi kwa sababu TUNADHANI Kuwa MUNGU ANACHELEWA, kumbe SIVYO, MUNGU HACHELEWI wala HAWAHI.

b) WATU WENYE MAUDHI:-
Hawa ni Watu TUNAOKUTANA nao katika maisha ya kila siku, iwe ni katika Familia au kwenye Ushirika KIROHO au KIMWILI Lakini WANAKWAZA,
- Mfano:- Wanafamilia, au Waumini wenzako, au Marafiki, au Ndugu, WANAWEZA KUKUKWAZA na USIPOANGALIA Unaweza KUONDOKA katika Uhusiano wako na MUNGU. Biblia inatuagiza Tuwaombee na Kuwakumbatia ili HURUMA YA MUNGU Iweze KUWABADILISHA na KUWAPONYA Vinginevyo UTAWACHUKIA. Biblia Inatuonya kuwa AMCHUKIAYE Ndugu yake ni MUUAJI hivyo USIWE na UCHUNGU na Wapendwa Wako. Bali OMBA IFUATAVYO:- “BWANA YESU HUYU NDUGU AMENIKWAZA LEO LAKINI UMESEMA NI MPENDE NA KUMWOMBEA. NINAONDOA KUMBUKUMBU ZOTE ZA MAKOSA YAKE, MOYONI MWANGU, KUANZIA LEO NINAMWOMBEA NA KUMPENDA. AMINA.”

Comments