BWANA ANA HAJA NAWE. *sehemu ya kumi*

Na mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana lipewe sifa…

Karibu tuendelee na fundisho hili,
lenye kufanyika Baraka kwa wengi ambao Bwana anazungumza nao kupitia mahali hapa,

*Kumbuka tulikoishia katika sehemu ya tisa,karibu sasa tuendelee;

Tazama mwana-punda huyo sasa,mara baada tu ya kutandikiwa nguo juu yake,
Biblia inatuambia kwamba WAKAMPANDISHA YESU.(Luka 19 : 35)
Hapo ndipo ninakokupenda sana jamani,wacha niseme jamani,
mimi nasema hapa hapa kwa kila mmoja…

Sikia;
Pindi walipompandisha Yesu,yule punda haukuonekana tena kama punda bali walimuona Yesu aliye juu ya punda…

Eeeh,jina la Bwana libarikiwe…
Maana katika mstari unaofuata tunasoma hivi ;
“Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani.” Luka 19 :36
Haya sikia tena,

Hapo mwanzo walizitandika nguo zao juu ya mwana-punda
(And they threw their own clothes on the colt, and they set Jesus on him.)Luka 19 :35
Sasa tunaambiwa habari nyingine kwamba ;
“Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani.” Luka 19 :36

Unasikia hapo,nasema hivi;
Wakatandika nguo zao chini,
acha ile juu ya punda .
Safari hii wakaziweka nguo zao chini ili mwana-punda huyo apite juu ya hizo nguo.

Maana yake ni kwamba,Hao watu walikubali nguo zao zikanyagwe na mwana-punda maana hawakumuona mwanapunda tena Bali walimuona Yesu ndie akanyagaye nguo zao,wakaendelea kumtupia nguo zao na kisha mwana-punda akazikanyaga tena kwa sababu amembeba Yeye mwenye mamlaka za kuzikanya hizo nguo.

Hivyo kwa sababu ni Bwana ndiye alieonekana kwa mwana-punda huyu,mwana-punda akaapewa heshima ya kipekee ambayo kamwe asing’eliweza kupata heshima ya namna hiyo,
Lakini kumbe alimbeba Yesu.

*Yawezekana huna heshima yoyote ile/Yaani huna kibali chochote kile,Lakini ninakuambia ukimbeba Yesu VIZURI,
kibali sio cha kuomba bali watu pamoja na falme zote zitajua kwamba zinastahili kuachilia kibali/heshima,

Kwamba famle zinastahili kuanguka mbele yako maana si wewe wakuangukiao bali waanguka kwa sababu ya Bwana Yesu uliyembeba.

*Kibali cha Bwana huja baada ya kumbeba Yesu yaani Bwana Yesu awe ndani yako.
*Kibali hakiombwi ndugu yangu,Bali ni zawadi ya Bwana kwa watu wake waliombeba Yeye vizuri.

Mwana-punda huyo kama ang’embeba Yesu kiupande-upande,yaani kana kwamba Yesu asing’epata nafasi nzuri ya kukaa vizuri juu yake ni dhahili kabisa ang’emdondosha Yesu,
Au hata kama asing’emdondosha lakini ikiwa Bwana Yesu kama asing’ekaa vizuri juu yake Basi watu wasing’etandika nguo zao juu yake hata chini yake.

Ila nampenda huyu punda maana aligundua siri hiyo kwamba ;
“ Inanipasa nimbebe Yesu vizuri,akae kwa kuenea vizuri,ndipo watu wataweza kutandika nguo zao ”

Sasa kanisa la leo halijagundua siri hii,kwamba siri ya kibali/mafanikio ni kumbeba Bwana Yesu vizuri,
na wala sio kumbeba tu,
kama kumbeba,
Bali kumbeba vizuri Yeye aenee,
ndipo mpenyo tutauona katika maisha yetu.

*Shida kubwa ambayo kanisa la leo linaikabili ni kwamba watu ambao Bwana ana haja nao,
wao hawana haja naye huyo Bwana,Ila leo Bwana ana haja nawe kwa ajili ya kazi yake ya utukufu.

Huyu punda asing’elipata heshima zote hizi kama asing’elikuja kwa Bwana Yesu,na sio kuja kama kuja tu Bali kumbeba Yesu…

ITAENDELEA…
• Kwa huduma ya maombezi juu ya jambo lolote lile,
Au kujuliana hali mawasiliano yangu ni
0655 111149,
0783 327375.
UBARIKIWE

Comments