BWANA ANA HAJA NAWE. *sehemu ya MWISHO*


Na mtumishi Gasper Madumla



Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana lipewe sifa…

Kumbuka msingi mkubwa wa fundisho hili ni kukuonesha kwamba Bwana ana haja na wewe,
kwa kuwa Yeye ndie aliyekuchaguaye wewe kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa (Waefeso 1: 4) kwa ajili ya utukufu wake uende mbele zake ukawe mtakatifu.

Andiko ambalo tumekuwa tukilisimamia kwa muda wote wa fundisho hili tangu kutoka sehemu ya kwanza hadi ya sehemu ya kumi,na hata katika sehemu hii ya leo ya mwisho,ni kutoka katika kitabu cha LUKA 19 : 29-38

Karibu tuendelee kidogo siku ya leo ;
Niliishia kwa kukuambia kwamba;

*Shida kubwa ambayo kanisa la leo linaikabili ni kwamba,watu ambao Bwana ana haja nao,
wao hawana haja naye huyo Bwana,Ila leo -Bwana ana haja nawe kwa ajili ya kazi yake ya utukufu.
Tazama andiko hili
Luka 19:29-38

*Huyu punda asing’elipata heshima zote hizi kama asing’elikuja kwa Bwana Yesu,na sio kuja kama kuja tu,
Bali kuja na kumbeba Yesu.

Sasa ipo gharama ya kumbeba Bwana Yesu Kristo,sio kitu cha rahisi-rahisi kama wengine wadhaniavyo.
Ni lazima ujikane nafsi yako ndipo uweze kuhiruhusu nafasi ya Mungu ikae ndani yako,kwamba chochote ufanyacho awe ni Bwana amefanya,
na sio wewe.

Hapo sasa ni kuyatenda mapenzi yake Bwana Mungu tu.
Kwa habari ya mwili wako unakuwa huhitaji kuhakiki matumizi ya mwili wako,kwa maana huo mwili si wa kwako bali ni wa Bwana,
wewe umepewa kama mkopo Biblia inatuambia ;

“Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE ;” 1 Wakorintho 6:19

Sikia hii tena;
Kwa habari ya mwana-punda,(Luka 19:29-38)
• Punda ndie aliyemuingiza Bwana Yesu Yerusalemu hiyo ni kweli,na vile vile ni Bwana Yesu ndie aliyemuingiza punda Yerusalemu.

Hapo utagundua kwamba kila mmoja ali-play part yake/alifanya kwa sehemu yake maana yake ni kwamba,Bwana Yesu alimuhitaji punda ili aingie Yerusalemu,

vile vile Punda alimuhitaji Bwana Yesu ili aingie Yerusalemu kwa sababu bila Bwana Yesu ukweli ni kwamba Punda asing’eingia Yerusalemu kwa sababu alikuwa amefungwa tena Bwana Yesu alimtumia punda kwa sababu punda naye alikubali kutumika.

Vivyo hivyo wewe ili uweze kuifikia Yerusalemu mpya(Mbingu ya tatu) unamuhitaji sana Bwana Yesu,naye Yesu anakuhitaji wewe achukue nafasi ndani yako,anahitaji utayari wako.

Jambo moja la msingi kati ya mabo mengi tuliojifunza hapa ni kwamba,;



• Bwana Yesu uachilia UPAKO kwa Yule aliye tayari kwa Upako huo,yaani Yeye humtumia mtu baada ya kuona utayari wa mtu huyo kutumika,
kama vile kwa habari ya mwana-punda maana tulisoma pale wanafunzi walipomfungua Punda,
Punda hakugoma kufunguliwa wala hakugoma kwenda kwa Bwana Yesu aliyekuwa anamuhitaji kwa ajili ya utukufu wake.

*Leo wapo watu ambao wameitwa kuifanya kazi ya Bwana lakini hawaifanyi kama vile kusudi la wito wao na hujikuta hukwama kila eneo maana Yule punda baada tu ya kufunguliwa tunaona kwamba akaenda kutumika kwa kazi ya Bwana ipasavyo na hapo watu wote hawakumuona tena Punda bali walimuona Yesu.

• Ukiona mpaka sasa upo mzima ujue Bwana ana haja nawe kwa kazi yake

• Ukiona afya yako ipo safi au hata kama inamatatizo bado Bwana ana haja nawe kwa kazi yake.

Bwana yupo tayari kumfungua mtu yeyote Yule ambaye anamuhitaji kwa kazi yake,na inawezekana ni wewe.
Anasema Yeye Bwana kwamba hata ile kukuwazia anakuwazia mawazo ya amani,
kukupa wewe tumaini tena zaidi ya yote anasema anakufundisha habari yake kwa ajili ya faida yako wewe mwenyewe.

Punda wa leo ni wewe uliyefungwa,
Kufungwa katika gereza la kukosa kibali,
Gereza la umaskini,
Gereza la kukosa nguvu za kiroho,N.K


Lakini leo Bwana Mungu amemtuma mtumishi wake hapa,kukueleza habari ya kufunguliwa kwako,
kwa sababu Bwana anakuhitaji ukaifanye kazi yake.
Kazi ya Bwana Mungu haifanywi na wachungaji tu ,
Au wainjilisti tu,
Au walimu tu,
Au mitume tu,
Au watenda kazi fulani hivi waliochaguliwa na kanisa tu,

Bali hufanywa na kila mtu mtu aliyekubali kwanza kufunguliwa kutoka katika vifungo vya namna nyingi,Pili ni yule aliyemkubali Bwana Yesu Kristo awe Bwana na Mwakozi wake,
tena ni mtu yule aliyefanya toba ya kweli kisha kumpokea Roho mtakatifu.

Hakuna jambo gumu la kumshinda Bwana Mungu wetu aliye hai,
Yeye,
“ Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki; ” Zab.146:8

Usiogope kuifanya kazi ya Bwana aliyekuitia,ifanye kwa ukamilifu naye atakuwa pamoja nawe siku zote kama vile ile habari ya mwana-punda.

MWISHO.
Mawasiliano yangu ni ;
0655-111149.
0783-327375.
UBARIKIWE.

Comments