BWANA ANA HAJA NAWE. *sehemu ya nane*

Na Mtumishi Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana lipewe sifa…

Haleluya…
Nasema Haleluya…

Nimepewa kazi moja tu na Bwana Mungu,nayo ni kuhubiri injili kwa watu wote,sina kazi nyingine yenye maana ambayo inampa Bwana utukufu,
isipokuwa ni kuhubiri injili tu.
Ndio maana leo Bwana kalileta neno lake hili mahali hapa kwa sababu Bwana ana haja nawe,ndio maana upo hai mpaka hivi sasa.

Nawe umepewa fursa hii ya pekee ya kupitia ujumbe huu,ujue lipo kusudi la Bwana ya kwamba Bwana ana haja nawe.
Msingi mkuu wa fundisho hili umetoka katika kitabu cha Luka 19 :31
Karibu tuzidi kuendelea zaidi kufundishwa na Roho wa Bwana mahali hapa;

Luka 19:31
'' Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, BWANA ANA HAJA NAYE ''

-Nilikuambia kwamba mwana-punda aliyefungwa ni Yule aliye chini ya sheria za mabwana zake,
yaani kwa lugha nyingine mwana-punda huyu ni yule anayetumikia sheria za mabwana zake ,
yupo chini ya sheria.
Ni mwana-punda asiyeelewa neno la haki.

Leo hii yupo mtu wa namna hii ambaye yupo chini ya sheria akiwatumikia mabwana zake,
na wala sio kwamba anamtumikia Mungu aliye hai.
Leo Bwana ana haja na mtu huyo,kwa sababu ikiwa ni ndio wewe, Bwana anataka kukutumia kwa ajili ya kazi yake.

Anakuhitaji wewe mtu mmoja ambaye umefungwa,
upo chini ya misingi ya dini,
ukitumikia dini pasipo kumtumikia Bwana Mungu kwa habari ya maisha ya wokovu.
Au yamkini umefungwa kwamba biashara zako haziendi, unafanya biashara kubwa kwa nguvu nyingi sana Lakini faida hupati,
nayo faida yako yote huchukuliwa na watu wengine waliokufunga
.
Muda huu lipo neno la Bwana mahali hapa kwa ajili yako.Au yamkini umekosa kibali kabisa kwa sababu U mwana-punda uliyefungwa,kwamba chochote ukifanyacho hakionekani kana kwamba umefanya,
Leo ipo Neema mahali hapa ya kukufungua ili ukatumike kwa kazi ya Bwana,

Labda tumuangaliye huyu mwana-punda aliyefungwa,na hapa Tunasoma habari zake

Luka 19 : 35-36;
“Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana-punda, wakampandisha Yesu.
Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani.”

Oooh haleluya…
Nilijifunza mengi kwa habari hii,Jina la Bwana libarikiwe…

*Biblia inatuambia kwamba Yesu alipowatuma wanafunzi wake wawili kwenda kwa mwana-punda mmoja aliyefungwa kwamba wamfungue, walimkuta kweli amefungwa nao wakamfungua kama Bwana asemavyo,
Na baada tu ya kumfungua Biblia inatuambia ;

“Wakampeleka kwa Yesu” (Luka 19:35)
hii ikiwa na maana kwamba yeyote anayefunguliwa ni lazima apelekwe kwa Bwana Yesu,kwa sababu hakuna mwanadamu mwenye kuweza kumfungua mtu aliyefungwa na nguvu za giza kwa kutumia nguvu zake binafsi,
isipokuwa kwa nguvu za Bwana Yesu tu,
nasema ISIPOKUWA KWA JINA LA YESU TU.

Hivyo hatuwezi kumfungua mtu yeyote kwa jina liwalo lote,isipokuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti tu,
na ndio maana wanafunzi wa Yesu baada tu ya kumfungua mwana-punda,
tunaona kitendo kinachofuatia ni kumpeleka kwa Yesu Kristo maana hata maandiko matakatifu yanatueleza kwamba ;

“ Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Matendo 4 :12.

Kwa lugha nyingine ni kwamba;
Yeye amfunguaye mtu kwa jina lingine ambalo sio la Bwana Yesu basi mtu huyo ni dhahili kwamba hakutumwa na Bwana Yesu,naye si mwanafunzi wa Yesu,
maana Biblia iko wazi kabisa kupitia andiko hilo ( Luka 19 :35a)

kwamba yeye ambaye ni mwanafunzi wa Yesu huenda kufanya kazi kwa kutumwa na Bwana Yesu,
wala sio kwa kujituma yeye mwenyewe,
tena mtu aliye mwanafunzi wa Yesu,
inampasa Kumpeleka huyo aliyefungwa kwa Bwana Yesu maana Yeye Yesu PEKEE ndio awezaye kumfungua kwa sababu anamuhitaji huyo aliyefungwa.

Tazama kwa makini andiko hilo lisemalo :
“Wakampeleka kwa Yesu…” Luka 19 :35a

Sikia,
Je waweza kujiuliza kwamba;
*Kwa nini wanafunzi wa Bwana Yesu walipotumwa kumfungua mwana –punda wasingempeleka kwa mwingine awaye yote?Bali ni kwa Yesu tu,?

ITAENDELEA…
• Kwa huduma ya maombezi juu ya jambo lolote lile,
Au kujuliana hali mawasiliano yangu ni
0655 111149,
0783 327375.

UBARIKIWE.

Comments