BWANA ANA HAJA NAWE. *sehemu ya nne. *

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

Karibu katika fundisho hili muhimu sana kwako,maana fundisho hili limekujia kwa muda na wakati sahihi ili Bwana ainuliwe,Na sasa tunaendelea katika sehemu ya tatu.

Luka 19 :29 ;
“ Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa Mizeituni, alituma wawili katika wale wanafunzi,”

Katika andiko hilo tunaona kuwa Bwana Yesu pamoja na wanafunzi wake wakiwa wamekaribia mlima wa Mizeituni,
Lakini Biblia haikutuambia kuwa idadi ya wanafunzi waliokuwa pamoja Bwana Yesu hapo walipokaribia katika mlima wa Mizeituni,
bali inatuambia kwamba Bwana Yesu aliwatuma wawili katika wale wanafunzi,

-Tazama hapo isemapo “alituma wawili katika wale wanafunzi,’’

Hii ikimaanisha kwamba walikuwa wanafunzi zaidi ya wawili na ndio maana tunasoma kwamba aliwatuma wawili kati ya wale wanafunzi.

Maana yake ni miongoni mwa wale wanafunzi wake,
Yeye aliwachagua wanafunzi wawili kwenda katika kijiji kinachowakabili kwa ajili ya kazi moja tru ya kumfungua mwana-punda mmoja aliyekuwa amefungwa.

Bwana Yesu hakuwatuma wanafunzi wake wote waende kumfungua mwana-punda aliyekuwa amefungwa,Bali aliwatuma wawili kati ya wanafunzi wake.

Bwana Yesu alitambua kwamba ipo tofauti kati ya karama ndani ya wanafunzi wake,Bali Roho ni Yeye Yule mmoja.

Maana wale wanafunzi wake aliowatuma walikuwa na karama za kufungua ambaye amefungwa,ndio maana baada ya kuwaangalia wanafunzi wake akawachagua wawili miongoni mwao wale wenye karama ya KUPONYA/KUFUNGUA.

Wale wanafunzi wengine si kana kwamba walikuwa hawana Yesu no! Walikuwa naye wote bali mafuta yao katika kazi ya Bwana yalitofautiana.
Leo wapo wanafunzi wa Bwana Yesu lakini sio wote wana karama za kufungua wale waliofungwa,

Wala hii haimaanishi kwamba hawana Yesu.
Maana andiko hilo hilo linatuambia kwamba
Luka 19:29;
“ Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa Mizeituni, alituma wawili katika wale wanafunzi,”
*Maana yake ni hii , wanafunzi wake waliokuwepo na Bwana Yesu ni wote au baadhi lakini si wote waliokuwepo naye wenye karama ya KUFUNGUA.

Haleluya…

Bwana ana aja nawe maana yeye anajua ipo karama gani ndani yako,na karama hiyo yatoka kwake yupo tayari sasa kukutuma katika kijiji kinachokukabili wewe kwa ajili ya kumfungua mwana-punda mmoja aliyekuwa amefungwa.

Kumbuka nilikuwambia kwamba neno Bethania ni neno lenye hasili ya lugha ya Kiyahudi lenye kuwakilisha nyumba ya maskini,
sasa nyumba si kama nyumba ya kawaida ya matofali na misumali,
Bali ni ukanda ulio wa kimaskini yaani ni eneo lililo la kimaskini.

Sasa karibu na maeneo hayo ndipo mwana-punda alipokuwa amefungwa.
Hapo utaelewa kuwa Yeye aliyefungwa hutawaliwa na umaskini.

Lakini leo Bwana akuambia ANA HAJA NAWE.
Maana Yeye aliuchukua umaskini wako na kukupa utajiri udumuo milele.

Sasa tazama hapa
Luka 19: 30

“ akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa.”

Hapa ni Bwana Yesu akiwatuma sasa wanafunzi wake kwa kuwaambia NENDENI maana yake hiyo ni AMRI sio hiyari.
Mtu akikuambia NENDA ni tofauti sana na akikuambia sasa WAWEZA KWENDA.
Hivyo walitumwa kama moja ya jukumu lao kwenda kumfungua mwanapunda aliyefungwa.

Wapo wanafunzi wa Bwana Yesu wa siku ya leo wameambiwa vivyo hivyo “NENDA”
Bwana Yesu akimaanisha kwamba kuwa mkristo ni jukumu la KWENDA kuwafungua wale wote waliofungwa nasema ni KWENDA hiyo ni sauti yake mwenyewe Yeye asema NENDA haikupasi kufikiri-fikiri bali NENDA Yeye atakuwezesha huko alikokutuma Yeye.

ITAENDELEA
• Kwa huduma ya maombezi juu ya jambo lolote lile au kujuliana hali mawasiliano yangu ni 0655 111149,0783 327375
UBARIKIWE.

Comments