BWANA ANA HAJA NAWE. *sehemu ya saba*

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana lipewe sifa…

Leo hii mimi nasema na maisha ya mtu mmoja mahali hapa,Ujumbe huu upo hapa kwa sababu Bwana ana kuhitaji wewe kwa ajili ya kazi yake aliyokuwekea tayari ndani yako uifanye.

Kumbuka nilikuambia kwamba ikiwa BWANA MUNGU akiwa na haja na mtu aweza kuachilia mateso kwa mtumishi wake ambaye amekesudiwa amlete mtu huyo kwa BWANA MUNGU,

na katika sehemu ya sita ya fundisho hili tuliangalia ni kwa namna gani wakina Paulo walivyo pata mapigo makali mara tu baada ya kumtoa pepo la uaguzi yule kijakazi ambaye alikuwa akiwapatia faida kubwa sana bwana zake.Baada ya hayo yote,

Mungu alikuwa ana haja na mlizi wa gereza kwamba aokoke yeye na nyumba yake yote,maana mara baada tu ya wakina Paulo na Sila kutupwa gerezani ndipo tunaona muujiza huu mkubwa ukitokea (Matendo 16:16-34)
(Soma zaidi katika sehemu iliyopita)
huo ulikuwa ni mfano mmoja ambao kama neno la Mungu lisemavyo katika kitabu cha Luka 19 :31

“ Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji ” Hivyo wakina Paulo na Sila waliulizwa-ulizwa kwamba “ Mbona mnafungua huyo kijakazi ?

Katika kuulizwa-ulizwa , wakajikuta wakipigwa na kutupwa gerezani kwa ajili ya kazi ya Bwana kwa sababu Bwana alikuwa ana haja na mlinzi wa gereza aokoke yeye na nyumba yake.

MFANO WA PILI,
• Stephano naye aliulizwa-ulizwa kwa habari ya kazi ya Bwana,naye katika kuulizwa-ulizwa wakampiga hata kuwawa,kwa ajili ya kazi ya Bwana kwa sababu BWANA ALIKUWA ANA HAJA NA INJILI YAKE IENDE KWA MATAIFA YOTE,MBALI NA YERUSALEMU TU.

Sikia hili;
Kabla ya kuuwawa kwa Stephano,injili ilikuwa ikihubiriwa Yerusalemu maana kanisa lilikuwa ni sehemu moja

,Wakina Petro na mitume wengine walilihudumia neno mezani,na kudumu katika fundisho sehemu moja,
Lakini mara baada tu ya kifo cha Stephano tunaona sasa Filipo ( Sio Yule Filipo mtume,

bali ni Filipo aliyechaguliwa kuwahudumia wanaweke wajane katika kanisa) akishuka Samaria na kwa akiwa amejaa Roho mtakatifu akikutana ana kwa ana na Simoni aliyekuwa mchawi,Na hatimaye tunaona Simoni naye akabatizwa ,akashikamana na Filipo.

Hivyo ulikuwa ni mpango wa Mungu wa kuuwawa kwa Stephano kwa sababu BWANA alikuwa ana haja na Simoni aokoke,ashikamane na Filipo,maana laiti kama Stephano asingelikufa kwa habari ya kuulizwa-ulizwa,(Luka :19:31)
kwa kupigwa hata kuuwawa basi Simoni hasingepokea wokovu kwa namna ile(Matendo 7:54-60,8:1-16).

Wala injili isingeenea kwa mataifa kwa haraka namna ile(Sisemi kwamba injili ising’efika kwa mataifa,Bali injili ing’efika lakini sio kwa haraka kama ilivyokuwa baada ya kifo cha Stefano)

Tunasoma sasa,
Matendo 8:14-17
“ Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;

kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.

Haleluya…
Jina la Bwana libarikiwe…
Ooh nampenda Yesu wa Nazareti...

Hakika Yeye ana haja nawe pia,kwa ajili ya kazi yake maana leo anakufundisha kwamba Yeye Mungu akiwa ana haja na mtu fulani,
anaweza kuachilia magumu yakupate wewe mtumishi wake kwa ajili ya kumpata mtu huyo mmoja mwenye haja naye.

Biblia inasema kwamba UTAULIZWA MASWALI JUU YA KAZI YA BWANA UIFANYAYO Kwamba ;
“ mbona wafanya mambo haya yote?Wafanya kwa mamlaka gani? ''
Katika maswali hayo yote kumbuka waweza KUPIGWA,
KUTUKANWA,
KUNENEWA VIBAYA KWA UONGO,
KUDHARAULIWA KATIKA JAMII KWA AJILI YA JINA LAKE BAWANA.N.K

maana maandiko matakatifu yatuambia tena;
“ Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.”
Mathayo 5 :11-12

Sasa angalia katika Andiko hilo Matendo 8:14-17
Tunaona mitume waliokuwa Yerusalemu wakishuka mpaka Samalia baada ya Filipo kuichapa kazi ya Bwana vizuri huko Samalia,ambapo Filipo aliweza kushuka huko kwa kusukumwa kwa habari ya mchafuko uliotokea huko Yerusalemu,

Na BAADA TU YA KIFO CHA STEPHANO ambapo Bwana alikuwa ana haja na Simoni aliyekuwa mchawi,
tena tazama Bwana akawa ana haja na MTU WAKUSHI,TOWASHI,lakini haya yote yalitukia baada tu ya kuulizwa ulizwa kwa Stephano hata kuuwawa,
kama tulivyosoma katika Luka 19:31.
Hivyo ulivyo,kwa Bwana wewe ni wa thamani ,hivyo anakuhitaji kwa kazi yake

Binti usichezee usichana wako,maana Bwana ana haja nawe,
Mvulana tunza uvulana katika Bwana,Kwa maana Yeye Bwana ana haja nawe…

ITAENDELEA…
• Kwa huduma ya maombezi juu ya jambo lolote lile,
Au kujuliana hali mawasiliano yangu ni
0655 111149,
0783 327375.

UBARIKIWE.

Comments