BWANA ANA HAJA NAWE. *sehemu ya sita *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla, 0655 111149


Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana lipewe sifa…

Leo hii mimi nasema na maisha ya mtu mmoja mahali hapa,Ujumbe huu upo hapa kwa sababu Bwana ana kuhitaji wewe kwa ajili ya kazi yake aliyokuwekea tayari ndani yako uifanye.

Yeye Bwana atakuwezesha maana atakutangulia kokote kule uendako,hujapopitishwa kwenye maji mengi lakini Yeye atakuwa pamoja nawe.
Na leo ameniagiza nikuambie kwamba BWANA ANA HAJA NAWE.
Katika kile kitabu cha Luka (Luka 19 : 29-38)ambacho ndio msingi mkuu wa fundisho hili, Leo tunasoma mstari wa 33 & 34.

Luka 19:33-34;
“ Na walipokuwa wakimfungua mwana-punda, wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwana-punda?
Wakasema, Bwana ana haja naye.”

Ona jinsi wanafunzi wa Yesu walivyoulizwa na jinsi walivyo jibu kama vile walivyoambiwa na Bwana.
Na vivyo hivyo itupasavyo kujibu pindi tuulizwapo na ufalme wa giza kwamba ;

“ Kwa nini unamfungua huyu tuliyemfunga?
Bwana anatuambia leo pindi tuulizwapo tujibu neno moja tu kwamba KWA SABABU BWANA ANA HAJA NAYE.

Nilikuambia kwamba wale wakuulizao maswali hayo sio wale walio upande wako,Bali ni wale walio kinyume nawe katika ulimwengu wa roho,wakiwa na nia ya kukukwamisha kiroho kwa kazi ya Bwana aliyoiweka ndani yako.

Katika kuulizwa-ulizwa kuna kupigwa,
Katika kuulizwa-ulizwa kuna kutukanwa ,
Katika kuulizwa-ulizwa kuna kutemewa mate,
Katika kuulizwa-ulizwa kuna kuuwawa kwa ajili ya kazi ya Bwana,N.K

Yote hayo hutokea kwa sababu Bwana ana haja na mtu mmoja apone kiroho.
Hivyo Bwana Mungu anaweza kuachilia maswali yakupate tena upigwe,utukanwe,udhalauliwe,hata kuteswa kupitia maswali hayo yote kwa sababu ya mtu mmoja ambaye Yeye Mungu anamuhitaji kupitia kwako.

Mfano;
Tuangalie mifano michache itakayo kusaidia;

Mfano wa kwanza ;
01.Matendo 16 :16,18-19
“ Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.

Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. ”

Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji;”

*Biblia inaendelea kuelezea vizuri namna ya wakina Paulo na Sila walivyotupwa gerezani kwa kupigwa sana,wakafungwa kwa mikatale,tena wakaaibishwa,wakateswa .N.K

Biblia inatuambia tena hapo mwanzo kabla ya kukamatwa wakina Paulo,baada ya kumtoa pepo la uaguzi yule kijakazi ndipo haya yote yakatukia,Lakini napenda ufahamu jambo hili kwamba;

• Hawakutiwa gerezani kwa sababu walimtoa pepo la uaguzi yule kijakazi,nasema NO,HAPANA!
Bali walitiwa gerezani na kuyapata mateso hayo yote kwa sababu Bwana Alikuwa ana haja na mlinzi wa gereza,kwamba AOKOKE tena na nyumba yake yote.

• Bwana aliachilia kuulizwa-ulizwa kwa akina Paulo na sila kwa sababu alikuwa na haja na mlinzi wa gereza amjue Mungu wa kweli aliyeumba mbingu na nchi,na alimuhitaji huyu mlinzi wa gereza kwa sababu ya kutangaza ufalme wake Mungu.

Watu wengi hudhani kwamba mateso waliyoyapata wakina Paulo na Sila yalitokana kwa kumtoa yule pepo la uaguzi kwa kijakazi.Haikuwa hivyo bali ni kwa sababu ya wokovu wa mlinzi.

Maana mlinzi wa lile gereza ange’okoka vipi pasipo kina Paulo kufika pale gerezani ?
Hivyo KUOKOKA kwa mlinzi kulikuwa mikononi mwa akina Paulo na Sila.

Haleluya…
Jina la Bwana libarikiwe…

Hayo mateso huyapatayo hivi sasa wewe mtu wa Mungu,yamkini Bwana ana haja na mtu mmoja ambaye ataguswa nayo,pale unapoendelea kusifu na kumtukuza Mungu kwa kazi yake,
muujiza wa Bwana upo ndani yako,utakaodhihilika kwako ili mtu huyo mmoja aokoke.

Biblia inatuambia kwamba wapo watu ambao watakuuliza-uliza wewe,
ambaye wewe uliyetumwa kufanya kazi ya Bwana,
Labda kwa kuudhiwa,
kuseng’enywa,
kupigwa kurushiwa maneno machafu,
kama akina Paulo walivyofanyiwa,Lakini Leo ninakuambia USIFE MOYO MAANA LIPO KUSUDI LA HAYO YOTE…

ITAENDELEA…
• Kwa huduma ya maombezi juu ya jambo lolote lile,
Au kujuliana hali mawasiliano yangu ni
0655 111149,
0783 327375.

UBARIKIWE.

Comments