![]() |
Mtumishi Gasper Madumla |
Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee kulitizama andiko hili ;
Luka 19: 30 ;
“ akisema, NENDENI mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa.”
-Hapa ni Bwana Yesu akiwatuma sasa wanafunzi wake kwa kuwaambia NENDENI maana yake hiyo ni AGIZO la kwenda kuifanya kazi yake.
Kumbuka hii,
Walipokuwa wamekaribia katika kijiji kinachowakabili mahali ambapo mwana-punda alipokuwa amefungwa,
Yesu na wanafunzi wake walikuwa hawajaingia ndani ya mji huo ambao yupo huyo mwana-punda,
Bali walikuwa wamekaribia tu huo mji,Lakini tunaona Bwana Yesu akaona mwana-punda aliyefungwa ingawa hakuwako huko mahali alipo mwana-punda huyo.
Hapa tunafundishwa kuwa;
• Yeye Bwana anakuona wewe kabla ya wewe kumuona Yeye,
Na ndio maana tunasoma hivi:
“kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.” Waefeso 1: 4
Kwamba Yeye alituona,akatuchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.Lakini sisi tuliochaguliwa, tumechaguliwa kwa kusudi moja tu kwamba tuwe watakatifu kwa utukufu wa Bwana.
Haleluya…
Jina la Bwana libarikiwe…
Bibilia inasema “ akisema, Nendeni mpaka kijiji kile “ KINACHOWAKABILI “…( Luka 19:30)
Neno hilo “Kinachowakabili “ katika Biblia ya New King James Version,(NKJV) limeandikwa hivi "Go into the village OPPOSITE YOU,…”
yaani ikimaanisha kwamba ;
Wanafunzi wa Bwana Yesu walitumwa kwenda kumfungua mwana-punda katika kijiji kilichokuwa kinyume nao,yaani ni kijiji ambacho kina kipingamizi. Hapo ni sawa sawa na neno katika Mathayo 10 :16;
“ Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.”
*Hivyo Bwana Yesu aliwatuma wanafunzi wake kama kondoo katikati ya mbwa-mwitu,
tena waende kufanya huduma ya kufungua yule aliyekuwa amefungwa.Na ndivyo tulivyo sisi wanafunzi wa Bwana Yesu wa leo,
tunafananishwa kama kondoo tuifanyapo kazi ya Bwana.
Ikiwa na maana kwamba ;
• Tumtegemee sana Yeye Bwana Yesu Kristo,
-hata katika maamuzi yetu yote tuongozwe naye kama vile alivyo kondoo,
ambaye hutegemea sana kuongozwa na mchungaji wake,
Maana kondoo kama utamuweka sehemu moja,
kisha ukaondoka,
ujue utakaporudi utamuona kabakia sehemu ile ile uliyomuacha,
akisubili umuambie maelekezo mengine,
Hivyo ndio maana tumefananishwa kama kondoo, kwamba yatupasa tuwe chini ya mchungaji wetu mmoja, Bwana Yesu kwa KUTII na KUISIKIA SAUTI YAKE KWA BIDII.
Mwana-punda wa leo ambaye Bwana ana haja naye ni wewe.
Yamkini umeteseka siku nyingi pasipo kufanikiwa kwa sababu upo katika gereza ;
Gereza la magonjwa,
Gereza la kukosa kibali,
Gereza la kutumikia sheria za dini na sio kumtumikia Mungu ipasavyo,
Gereza la udhaifu,N.k
Lakini leo yupo mmoja awezaye kukusaidia naye ni Yesu Kristo wa Nazareti,kwa sababu Yeye anakuhitaji kwa ajili ya kazi yake aliyokuwekea tayari.
Kwa habari ya mwana-punda,Biblia inatueleza kwamba, wanafunzi wa Bwana Yesu watakapoulizwa
“ Mbona mnamfungua ?“ wao wajibu hivi;
“Bwana ana haja naye”
Ikimaanisha kwamba katika kuifanya kazi ya Bwana kwa kuwaendea wale waliofungwa,
basi kupo kuulizwa,Ipo hali ya kuulizwa juu ya kazi uliyotumwa na Bwana kuifanya.
Kwamba ;
“ Mbona wafanya hivi ?”
“ Kwa mamlaka gani unayatenda haya?”
“ Je ni kweli mtu aweza kupona?”
“ Je wewe sio agent wa shetani,?inawezekanaje yeye asiyeweza kutembea, akatembea?N.K
*Sasa tumeambiwa kwamba pindi watakapokuuliza hivyo wewe uwe na jibu moja tu kwamba,KWA SABABU BWANA ANA HAJA NAO.
Wakuulizao sio wale mliopo pamoja katika huduma ya Bwana, bali ni wale walio kinyume na wewe katika ulimwengu wa roho.
Ibilisi na majeshi ya mapepo na ufalme wao ndio watakuuliza wewe mwana funzi wa Yesu kwamba “ Mbona unamfungua?,huyu mali yetu,!!”
ITAENDELEA…
• Kwa huduma ya maombezi juu ya jambo lolote lile,
au kujuliana hali mawasiliano yangu ni ;
0655 111149,
0783 327375.
UBARIKIWE.
Comments