BWANA ANA HAJA NAWE. *sehemu ya tisa*

NA MTUMISHI WA MUNGU, GASPER MADUMLA


Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana lipewe sifa…

Kumbuka tulikuwa tumeishia hapa;
“Wakampeleka kwa Yesu…” Luka 19 :35a

Sikia,
Je waweza kujiuliza kwamba;
*Kwa nini wanafunzi wa Bwana Yesu walipotumwa kumfungua mwana –punda wasingempeleka kwa mwingine awaye yote?Bali ni kwa Yesu tu,?
Jibu lake;

Waligundua siri hii,
kwamba mwanadamu yeyote hana mbingu ,
hivyo wakapiga hesabu na kuona kwamba yupo mmoja aliyewatuma kufanya kazi yake ambaye kwa huyo ipo mbingu.
Hakuna mwenye kukusaidia kukupa mbingu hata kama ni mchungaji wako au,
Hata kama ni Papa/pope,au
Hata kamani askofu,N.K
Wote hao,nao wanahitaji mbingu,hivyo hawawezi kukupa kitu wasichokuwa nacho.

Lakini wewe mpendwa Bwana ana haja nawe akutumie kwa utukufu wake sababu ni Yeye pekee mwenye mbingu.

Tazama tena Luka hiyo hiyo 19 mstari wa 35 “
Luka 19 :35;
“ Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana-punda, wakampandisha Yesu.”

Huyu mwanapunda mara tu baada ya kupelekwa kwa Bwana Yesu Biblia inaendelea kutuambia kwamba;

“…wakatandika nguo zao juu ya mwana-punda,”…..Alafu/then hajaishia hapo tu, tena Biblia inatuambia kwamba “ wakampandisha Yesu.”

*Watu walikubali kutandika nguo zao kwa mwana-punda,hili ni jambo la ajabu sana. Kwa sababu pata picha sasa ya punda aliyefungwa kwa kitambo fulani,
kwamba ni lazima alikuwa ana harufu mbaya sana ya mikojo au kinyesi kwa sababu alikuwa amefungwa sehemu moja tu.

Na ndivyo ilivyo hata mtu aliyefungwa kiroho kwa mapepo wachafu,kiroho mtu huyo si msafi hata kidogo,na ndio maana Roho mtakatifu hawezi kufanya makao kwa mtu huyo mwenye uchafu kwa sababu Yeye Roho ni mtakatifu sana.

Okey,
pata picha hiyo,kwamba punda huyo ni lazima alikuwa mchafu sana lakini Biblia inatuambia kwamba alipopelekwa tu kwa Yesu,gafla watu wakatandika nguo zao juu yake.
Hii ikimaanisha kwamba pindi alipofunguliwa uchafu haukuonekana tena na ndio maana hata watu wakatandika nguo zao juu yake.

Vivyo hiyo yeye aliyekuwa mchafu wa dhambi,kwa sababu ya kufungwa na mapepo,Gafla mtu huyo akifunguliwa vifungo hivyo,kwa habari ya toba ya kweli,basi uchafu wa dhambi hauna nafasi tena,na kamwe hautaonekana.

Sikia jambo hili tena,
*Ni jambo gumu kwa akili za kibinadamu kueleweka kwa habari hiyo ya mwana-punda pale watu walipotoa nguo zao kwa kuzitandika juu ya mwana-punda.

Maana mtu aweza sema “ Ya nini haya yote,?maana nguo zangu hizi ni safi yanifaa nini kuzitandika juu ya mnyama huyu? ”

Lakini sivyo hivyo kwa habari ya mwana-punda ambaye Bwana ana haja naye,Watu hawa waliotandika nguo zao hawakujiuliza-uliza maswali bali waliweza kuzitandika nguo zao kwa sababu Bwana ana haja naye.

• Kutandikiwa nguo kiroho ni jamba la heshima ya pekee kwa Yule asiyestahili.

Maana mwana-punda huyu alikuwa astahili kutandikiwa nguo,tena asingeweza kupata heshima hiyo yote.
Lakini baada tu ya kupelekwa kwa Yesu, akatandikiwa nguo juu yake.
Maana hawakumuona kama punda yule aliyefungwa,

Bali walimuona Yesu sababu alikuwa na sura nyingine baada ya kufunguliwa kutoka katika kifungo,
Vivyo hivyo mtu anapokuwa katika vifungo huwa na sura nyingine tofauti na sura atakayo kuwa nayo mara tu baada ya kufunguliwa hivyo vifungo.

Nami sasa nasema na mtu mmoja mahali hapa,na yawezekana ni wewe kwamba hivi sasa una sura nyingine ambayo kiukweli kabisa sio sura yako,ambayo kwa sura hiyo umekosa KIBALI.

Tazama mwana-punda huyo sasa,mara baada tu ya kutandikiwa nguo juu yake, Biblia inatuambia kwamba WAKAMPANDISHA YESU.(Luka 19 : 35)

Oooh.. Haleluyaaa…
Oooh!.. Haleluyaaa…

ITAENDELEA…
• Kwa huduma ya maombezi juu ya jambo lolote lile,
Au kujuliana hali mawasiliano yangu ni
0655 111149,
0783 327375.
UBARIKIWE.

Comments