BWANA ASEMA,YATOSHA, SASA NI WAKATI WAKE KUONEKANA.

Sospeter Simon S. Ndabagoye


Mlivyozunguka mlima huu,"Vyatosha"; geukeni upande wa kaskazini.Nawe, waagize watu,uwaambie,Mtapita kati ya mpaka wa ndugu zenu...nao watawaogopa....sitete nao,kwa maana sitawapa katika nchi yao kamwe...(Kumbukumbu la Torati 2:3-5)

Sijui, umekua katika hali hiyo uliyonayo kwa muda gani, wala sijui umehangaishwa na hiyo hali kiasi gani,ila leo Mungu anasema YATOSHA.
Pengine umeonewa sana, Umedharauliwa sana, Umetukanwa, Umekatishwa tamaa, Umebezwa kwa kila jambo, Umetemewa mate, Umechukiwa na hata Kutengwa na jamaa,Umepuuzwa mno, ila leo Mungu anasema"YATOSHA"

Haijalishi umeugua kwa muda gani, Umetafuta kazi pasipo kupata kwa muda gani,Umevumilia ili upate mwenzako kwa Muda gani? ila leo Mungu anasema "YATOSHA" Wakati wako wa kukumbukwa ni sasa, hata kama umeteswa na ulevi, uchawi,uzinzi,masengenyo n.k., Wee geuka upande wa pili, Mgeukie Yesu sasa, na hao adui zako watakuogopa, wala hawatakuwa na nafasi ya kuendelea kukutesa.
Hayo Magonjwa yatakuogopa, huo umalaya utakuogopa, adui sigara, pombe na wizi, vitakuogopa, wee geuka upande wa pili, mwangalie aliyekufa msalabani kwaajili yako, na hilo unaloliona tatizo kwako,litakuogopa hata litakukimbia.

Kama vile Mungu alivyowakumbuka Wanawaisraeli, walipokuwa wakiizunguka nchi ya Edomu,walipokuwa wamekufa moyo,wamekata tamaa,hata wakafikiria Mungu amewaacha, wengien wakadhani wamemtenda dhambi, hata wakaanza kukufuru na kulalamika (Hesabu 21:4-9). Hata wewe Mungu leo anaona maisha unayoishi, anaona changamoto unazokumbana nazo. Haijalishi ni kwa muda gani umekaa katika hali hiyo, ila Mungu anasema Yatosha, umefika wakati wake kuonekana katika maisha yako ikiwa utakubari kumgeukia na kufuata njia zake.
Hakika na kwambia,hutajuta kumgeukia,wala hutakuja kunyanyaswa ukimwamini.

NAKUTAKIA BARAKA ZA BWANA MAISHANI MWAKO, AKOMESHE MATESO YOTE,AONDOE ADHA ZA KILA NAMNA,ASIYE NA MTOTO APATE MTOTO,ASIYE NA KAZI APATE, AWAINUE KATIKA KAZI ZENU,BIASHARA ZENU, NA ZAIDI AWAJARIE AFYA NJEMA NA MAFANIKIO DAIMA.

Comments