Dotnatha ajenga Kanisa lake.


Dotnatha
STAA wa sinema za Kitanzania,  Illuminatha Poshi ‘Dotnatha’ amejenga kanisa lake, Bomba Mbili, Ukonga nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo anatarajia kulizindua hivi karibuni baada ya kukamilisha vitu vyote muhimu.
 
Akizungumza na gazeti hili, Dotnatha alisema amekuwa haonekani mara kwa mara kutokana na  kutingwa na shughuli mbalimbali za ‘kulisimamisha’ kanisa hilo pamoja na kwenda shule kusomea taaluma ya  Biblia ili kujiweka katika nafasi muhimu ya kuongoza wanakondoo wa Bwana.
 
“Kanisa langu linakadiriwa kuchukuwa watu wapatao 2000 kwani ni kubwa na litakuwa likihudumiwa na wachungaji mbalimbali, ambao watakuwa wakipita kwa ajili ya kuongoza akiwemo Nabii Flora, ” alisema Dotnatha.
 
Hata hivyo, msanii huyo hakusita kutoa shukurani zake kwa muumba wa mbingu na nchi kwa kumuwezesha kutimiza ndoto zake za muda mrefu, bila kusahahu jitihada za mumewe, Mohamed Posh ambazo ni pamoja na ushauri wa karibu.

- Global Publishers -

Comments