FAHAMU NAFASI YAKO KATIKA UKRISTO.

Mtumishi Gasper Madumla
Bwana Yesu asifiwe...
Watu wengi hawafahamu nafasi zao katika maisha ya ukristo. Kuwa mkristo maana yake ni kuwa mwanafunzi na mfuasi wa Kristo ambaye Yeye ndio dira yetu.
Ikiwa Yeye mwenyewe Kristo Yesu,dira yetu alisimama vizuri na Mungu Baba kwa kuwafungua wale wote waliokuwa wameonewa na kuteswa vikali na falme za giza,
Basi nasi yatupasa kutembea humo alikotembea dira yetu,pasipo kujali kwamba watu watatuonaje.

Leo wapo watu waishio nje ya kituo chao. Maana wengine wapo sehemu ambazo hawastahili kuwapo katika hizo sehemu,hao sasa wamekuwa ni nje ya kituo chao.
Yamkini muda huu wewe ungelitakiwa uwe madhabahuni kwa kazi ya Bwana,lakini galfa unajikuta upo bar. Yamkini ungelitakiwa muda huu uwepo katika maombi ya kuombea familia yako,
Lakini kumbe upo unasengenya mahali fulani.

Imefika wakati sasa wa kwenda mbele za Bwana kwanza kwa toba kisha kuuliza juu ya kazi gani ambayo Bwana amekuitia kuifanya
Sababu kukaa nyumbani mwa Bwana bila kazi ya kufanya ni jambo baya sana.

UBARIKIWE.

Comments