![]() |
Na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima|Kawe Tanganyika Packers|Dar es Salaam |
1.0 Utangulizi
Leo nitafundisha kwa
habari ya ndoto. Neno ndoto limeandikwa ndani ya Biblia zaidi ya mara 86.
Katika kitabu cha mwanzo pekee neno ndoto limeandikwa zaidi ya mara 30. Katika
kitabu cha Daniel neno ndoto limejitokeza zaidi ya mara 22.Kwa kawaida kila
andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho.
Nitafundisha hatari ya
ndoto leo kwa mifano ya ndoto za wafalme wawili. Mfalme wa kwanza Nebukadreza
aliyekuwa mfalme katika mashariki ya kati. (Danieli 2:1-6) Nebukadreza
alitawala kipindi ambacho ufalme wake ulikuwa mkubwa mashariki ya kati yote na
dunia yote. Mfano wa pili ni mfalme wa Misri Farao, huyu alikuwa mfalme katika
Afrika (Mwanzo 41:1-8).
Daniel 2: 1-6, tunajifunza
habari ya ndoto iliyootwa na Mfalme Nebudkadreza. “ Hata katika mwaka wa pili
wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake
ikafadhaika, usingizi ukamwacha….”
1.1 Ndoto
ni nini?
Ndoto ni jambo
linalotakiwa kumpata mtu siku chache zijazo. Ndoto ni kipimo cha hali ya rohoni
ya mwotaji. Mfano mtu akiota anakimbizwa na ng’ombe inaamanisha kuwa kiwango
cha nguvu zako za rohoni kimeshuka. Endapo utaota wewe ndio unamkimbiza adui
inamaana nguvu zako za rohoni zipo juu. Ndoto ni bayana.
2.0 Msisitizo
wa Hatari ya ndoto
Ikiwa ndoto inamfadhaisha
mfalme ambaye ni mkuu wan chi, je nini mimi na wewe? Hii inatuonesha kuwa
kitendo cha mfalme kutaka kufahamu tafasiri ya ndoto inamaanisha kuwa ndoto ni
bayana.
2.1 Mambo
ya kufanya ukiota ndoto
(i) Jambo la kwanza la
kufanya baada ya kuota ndoto ni kuindika
hiyo ndoto
Habakuki 2:2-3; BWANA
akanijibu akasema, iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili kila
aisomaye apate kuisoma kama maji.
(ii) Baini je ndoto
uliyoota ni ya mema au ya mabaya
(iii) Ukiota ndoto
ukabaini ni ya mabaya anza kuomba mara baada ya kustuka toka ndotoni.
Usisubirie kukuche. Omba kinyume cha hiyo ndoto. Batilisha hiyo ndoto.
2.2 Maandiko
yanayofanya baadhi ya watu wapuuzie ndoto
Mhubiri 5:3; “kwa maana
ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi…”
Zekaria 10:2; “kwa maana vinyago
vimenena maneno ya ubatili nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za
ndoto za uongo…”
Yeremia 23:25; “Nimesikia
waliyosema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema nimeota ndoto
nimeota ndoto.”
Watu hupuunza ndoto kwa
kuwa ndoto huja kwa shughuli nyingi na pia hupuuza ndoto kwa kuwa zipo ndoto za
uongo. Kimsingi kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho. Uwepo wa
maandiko mawili yanayofanya baadhi ya watu wapuuzie ndoto hauwezi kupuuza ndoto
zaidi ya 80 ambao zilikuwa bayana, na Mungu alisema na watu katika ndoto.
3.0 Baadhi
ya maandiko yanayotufanya tuzishughulikie ndoto tunazoota
Mwanzo 20:3-5; “Lakini
Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku…”
Mwanzo 28:12 Ndoto ya
Yakobo “…akaota ndoto na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake
yafika mbinguni. Tena tazama malaika wa Mungu wanapanda na kushuka juu yake….”
Mwanzo 31:11”Na malaika wa
Mungu akiniambia katika ndoto…”
Mwanzo 31:23-24 “…Mungu
akamjia Labani Mshami katika ndoto ya usiku…”
Mwanzo 37:46; ndoto ya
Yusuph
1 Falme 3:5-10; Ndoto ya
Suleiman
Comments