![]() |
Mwili wa Marehemu ukiingizwa Kaburini |
Leo ndo ilikuwa ndiyo siku ya Mwisho ya
safari ya Askofu Dr. Mosses Kulola, safari iliyohitimishwa kwa Mwili
wake kupumzishwa katika nyumba yake ya milele.
![]() |
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu likiwa Kaburini |
Mazishi yake yamefanyika katika Kanisa
la EAGT Bugando na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na
Makanisa mbaimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Jakaya Mrisho
Kikwete.
![]() |
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete |
Viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja
na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Engeneer Evarist Ndikilo, Waziri Mkuu Mstaafu
Edward Lowasa, Katibu Mkuu wa CHADEMA Wilbroad Slaa, Mbunge wa
Nyamagana(CHADEMA) Ezekiel Wenje.
![]() |
Edward Lowasa akiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu |
Pia Waimbaji mbalimbali wa Nyimbo za
Injili Tanzania walikuwepo kuhakikisha kuwa zoezi zima linaambatana na
Nyimbo mbalimbali za kumuenzi Baba/Babu yetu Askofu Dr. Mosses Kulola.
![]() |
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete |
Sasa naomba nikukumbushe Wasifu wa
Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola uliosomwa Jana katika Uwanja wa CCM
Kirumba wakati wa kutoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu.
Comments