"IKIWA WEWE UNAPENDA KUWA MKRISTO WA KWELI WA KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU VITAMBUE NA KUVIEPUKA VITU HIVI VIMCHUKIZAYO MUNGU"

Na Abel Suleiman Shiriwa

Mithali 6:16-19
16 Kuna vitu sita anavyovichikia BWANA;
Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.

Macho ya kiburi, Ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 Moyo uwazao mawazo mabaya;
Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;

19 Shahidi wa uongo asemaye uongo, Naye apandaye mbegu ya fitina kati ya ndugu.
(1) Jieupushe na Kiburi.
Mithali 16:5 Kila mwenye moyo wa kiburi ni machukizo kwa BWANA;
Hakika, hatakosa adhabu.

(2) JIEPUSHE NA UONGO.
Mithali 16:22 Midomo ya uongo ni Machukizo kwa BWANA;
Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.

Ufunuo 22:15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
(3) IEPUSHE MIKONO YAKO KUMWAGA DAMU.
Isaya 1:15-16
15 Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
16 Jiosheni, Jitakaseni, ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele ya macho yangu; acheni kutenda mabaya.
(4) ZUIA MOYO WAKO KUWAZA MAWAZO MABAYA.
Yeremia 17:9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Marko 7:21-23
21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.
(5) IKIMBIE ZINAA.
1 Korintho 6:18 Ikimbieni zinaa, Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake, ila yeye afanyae zinaa hufanya juu ya mwili mwenyewe.
(6) USIWE SHAHIDI WA UONGO.
Mithali 19:9 Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;
Naye asemaye uongo ataangamia.

(7) JIEUPESHE KUPANDA FITINA..
Walawi 19:16 Usiende huko na huko katikati ya watu wako kama mchongezi; wala usisimame kinyume na damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.
MUNGU AKUBARIKI UNAPOUTAKAFARI UJUMBE HUU NA UNAPOCHUKUA JUKUMU LA KUUFANYIA KAZI...
AMEN!

Comments