JE, NANI MKWELI JUU YA KIFO KATI YA MUNGU NA IBILISI?



Lengo kuu: Kubambanua ukweli juu ya kifo na asili yake.
Lengo Mahususi: Kung’amua ukweli uliofichika juu ya kifo na lini kilianza.

(a) Utangulizi.
Kifo ni nini?
Ni hali ya kutokuwa na uhai. Tukio hili,humfikia kiumbe pale uhai unapokoma. Kiumbe huyu anaweza akawa mnyama,mdudu au mmea. Kitendo cha kufa,huwa ndiyo kikomo cha tabia zote za uhai. Aghalabu, uhai unapokoma, maendeleo ya ukuaji yote huishia hapo, na kuanza hatua nyingine ya kuharibika kwa mujibu wa uthibitisho wa kisayansi japo kiimani, kifoni mwanzo wa maisha yaliyo katika mfumo mwingine wa kiroho.
Tunayaona hayo katika (Luka 16:19-31)tunaposoma habari za Tajiri aliyeishi kwa anasana na Lazaro aliyeishi kwa taabu sana, lakini akiwa mcha Mungu; tunaona baada ya kufa kwao wote, walikuja kukutana. Lakini pia (Luka 23:42&43) pale msalabani, tunamwona Yesu akimwahidi mwizi aliyetubu,kuwa watakuwa pamoja mbinguni(bila shaka, ni baada ya kifo chake) pia (2Wakorintho5:1-10) tunajifunza habari juu ya nyumba za kiroho,nyumba zisizoharibika,nyumba zilizoanadaliwa kwaajili ya makazi ya milele, makazi yanayoaanza baada ya makazi ya duniani kuisha. Na (1Petro3:18-20) inatupa habari za kukoma kwa uhai wa Yesu duniani kupitia msalaba,ambao kwao umefanyika ukombozi kwa watu wote.
(b) Kiini cha Somo.
Baada ya kuchunguza kwa ufupi utangulizi huo, ebu turejee kwenye mada yetu ya leo; pengine umeshangazwa na Kichwa cha mada hiyo, kwa kuwa inajulikana wazi kuwa Shetani,ni baba wa Uongo,ndiyo maana anaitwa Ibilisi,aundanganyae ulimwengu wote,kwa hila na ghadhabu nyingi.
Biblia inatuonesha kila kilichotokea bustanini mwa Edeni, baada ya Adamu na Eva kushindwa kuishi kwa kufuata maelekezo aliyowapa. Na hapa, ndipo tunapotegemea kuona, adhabu ya kifo ikianza kufanya kazi kwa kuwa,wamevunja agizo la Mungu. Kwa hali ya kawaida, Kuvunjwa kwa sheria, kunairuhusu adhabu iliyondani yake kutekelezwa. Kadharika, kwa kunjwa kwa agizo la Mungu, tunategemea kuona msiba mkubwa ukitokea kama Mungu alivyosema.
“BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema,matunda ya kila mti wa busatni,wewaza kula; Walakini, matunda ya mti wa ujuzi na mema na mabaya usile; kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo,utakufa hakika”(Mwanza 2:16&17).
Cha ajabu, shetani alipokuja kumjaribu Eva, alimpa kauli tofauti na lile agizo la Mungu.
“....Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu,Msile matunda yote ya bustanini?.....Mwanamke akasema, matunda ya miti ya bustanini twaweza kula,isipokuwa mti wa ulio katikati ya bustani....Mungu amesema msiyale,wala msiyaguse mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke; Hakika, hutakufa” (Mwanzo3:1-4).
Kutokana na maagizo ya Mungu, tunategemea kuona Adam na Eva uhai wao ukikoma baada ya kwenda kinyume na maagizo ya Mungu, badala yake, tunaona wakipewa adhabu nyingine ikiambatana na laana na uadui kujengwa kati ya nyoka na mwanadamu.(Mwanzo 3:14-19)
La kujiuliza ni Je, hii ndiyo ilikuwa adhabu ya Mungu tangu awali au alibatilisha, kama alibatilisha!Je, shetani hakuwa mkweli aliposema “hakika, hamtakufa”
Misitari hiyo, imekuwa ikiwachanganya sana wasomaji wengi wa Biblia hata wachambuzi mbali mbali ; wengine wamemuunga mkono shetani kuwa alisema ukweli,wakati wanajua kabisa kuwa ni baba wa uongo, na wengine wamefikia hatua ya kuamua kuacha bila fuatilia kwa kina juu ya maaneno hayo na kusingizia kile kilichoandikwa katika (Kumb. la Torati 29:29) kuwa” Mambo ya siri ni ya Bwana.......lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu........
Ndugu yangu, hakuna neno liwalo lote, ambalo Bwana Mungu amelificha hata asiwahabarishe wamchao; Tendo la Adamu na Eva kula tunda, ni zao la kazi ya shetani, la kuudanganya ulimwengu, na hili linadhirisha wazi kuwa, shetani alitupwa duniani kabla ya Adamu kuwako, ndiyo maana, alipomjaribu Eva, aliweza kusema japo kwa kugeuza yale maagizo aliyotoa Bwana Mungu juu ya ulaji wa matunda.
Lengo la shetani, ilikuwa kuwadanganya ili wafe. Tukio hili,lingempatia nafasi yeye zaidi ya kuwa mtawala wa dunia, kinyume na mpango wa Mungu wa kumuumba mwanadamu. Kwa kuwa Mungu alimuumba mwanadamu ili atawale vitu vyote alivyoviumba, na shetani mwenyewe akiwemo, kwa kuwa yeye kadharika aliumbwa na Mungu (Mwanzo1:25-27).
Kinacholeta utata wa nani mkweli katika tamko la kufa au kutokufa baada ya kula tunda, ni “MUDA” Wasomaji wengi, wanaposoma andiko hilo,wanategemea kuona Adamu na Eva wakifa baada ya kula tunda. Pengine hata shetani,alishangaa sana,kuona hawajafa mpaka Mungu anakuja na kuchukua hatua nyingine tofauti na alivyotarajia, wakati yeye alijua hiyo ni sumu ya kuwamaliza kabisa.
Ndugu msomaji, tukio la kufa alilolisema Mungu, hakulifunga ndani ya muda flani( halina time limit); Yeye alichosema, ni kuwa “....msile wala kuyagusa mkafa....” hiki hiki,baada ya kula tunda alikirudia katika (Mwanzo 3:19)”.....hata utakapoirudia ardhi....kwa maana u mavumbi wewe,nawe mavumbini utarudi” maneno haya,yanatupa ushahidi tosha kuwa, Mungu aliendelea kusisitiza kile alichoeleza tangu awali,alipokuwa anawaweka bustanini kabla ya kudanganywa hata kumwasi.
Kuwa, ....matunda ya kila mti wa busatni,wewaza kula; Walakini, matunda ya mti wa ujuzi na mema na mabaya usile; kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo,utakufa hakika”(Mwanza 2:16&17).
Ifahamike kuwa, uongo wa Ibilisi,hauwezi kuondoa mpango wa Mungu. Kwa maneno mengine ni kwamba, haraka za shetani za kutamani kutawala,haziwezi kuondoa mpango wa Mungu wa mwanadamu kutawala. Hatahivyo, shetani hawezi kujitapa kuwa ameshinda kwa kutengua neno la Mungu kwa kuwa wamekula na hawajafa. Lazima tuelewane hapa.
Adhabu ya Mungu ya kufa, tunaiona ikitimia kupitia uzao wa Adamu; ambapo Habili anauawa na nduguye Kaini (Mwanzo 4:8). Tendo hili la mauaji,linatimiza adhabu ya kifo aliyosema Mungu, na msiba huu wa kwanza kuwepo tangu kuumbwa kwa dunia, hapana shaka, uliacha simanzi kubwa sana, na pengine hata, ingekuwa vigumu kuelewa kitu kinachoendelea kwa kuwa, hakuna aliyekuwa anafahamu hali inayokuwepo mtu anapokuwa amekufa. Labda ulitumika uzoefu wa kupitia wanyama wengine.
Licha ya kuwa Kaini,alinyoshewa kidole kuwa amemuua ndugu yake, pegine Hawa(Eva kabla ya kula tunda) alikumbuka mbali zaidi kwenye agano lao na Mungu,kuwa wakilia tunda, kifo kitawafika. Ndiyo maana tunaona, Adamu akimhoji Kaini, kuwa nduguye yuko wapi, lakini hatuoni Hawa akihoji jambo lolote.
Tangu hapo, vifo vimeendelea kuongezeka mpaka leo kutokana mtu mmoja Habili, mpaka maelfu na maelfu na mpaka sasa lililo andiko la Mungu linatimia.
(c) Hitimisho.
Natumai umeelewa sasa, na somo hili limekuvusha kiwango cha zamani. Endelea kumwomba Mungu akufunulie zaidi. Kwani wote tunajua kuwa kifo kipo, na hata sisi tunafahamu kabisa kuwa, tutakufa siku moja, ndugu zetu, watoto wetu na hata marafiki zetu, watakufa. Ila cha kujihadhari ni kuhakikisha, tunakufa katika utakatifu. Kifo chenye faida. Paulo anasema”Kuishi ni kristo, ila kufa ni faida” lakini, sharti ujue kuwa si vifo vyote ni faida, bali vifo amabovyo unakufa huku ukiwa mtakatifu. Na kwa kuwa kifo hakina subira, kama tulivyoona kua Habili alikufa ghafla, hata leo vofo hivi vipo, kuna vifo vya ajari, vofo vya ugomvi, hasira, kutekwa na kuuawa n.k. hivyo, kama askari vitani, unaswa kuwa tayari muda wowote,kwa maana hujui muda wala saa na aina ya kifo.
Mungu atusaidie wote, tuwe tayari kwa majira tujuwayo, nayo tusiyojua. Amen.

Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries (NEM-Tanzania)

Comments