![]() |
Na mtumishi wa MUNGU Mchungaji na Mwl Peter Mitimingi |
11. Ni watu Wenye Ujasiri Mkubwa Sana.
Sangwini ni watu wenye ujasiri mkubwa sana. Huwa hawaogopi kuongea, hawaogopi kujitokeza mstari wa mbele, wanaujasiri mkubwa wa kujitokeza mbele kukabiliana na yeyote au chochote. Mwanaume ambaye ni Melankoli ambaye ameoa mke Sangwini usiku nyumbani akitokea nyoka mwanaume atakuwa anakimbia kurudi nyuma na mke wake atakuwa anakimbia mbele kukabiliana na huyo nyoka na mume yeye atabakia kumuhamasisha mkewe pigaa, pigaa, mkanyage kabisa mpaka afe, ila yeye hatathubutu kumsogelea. Sangwini hawaogopi kusimama mbele ya umati wa watu na kucheza au kuongea kwenye kadamnasi.
12. Mara nyingi sio watu wa kuwekea sana jambo moyoni.
Sangwini hana chumba cha kuhifadhi mambo moyoni kwa muda mrefu. Anakasirika kwa haraka sana na hasira zake zinaisha kwa haraka sana kwasababu ya ile sifa ya misisimko. (emotion) misisimko yake ikishuka tu na hasira zinashuka pia anarudi kuwa kawaida kabisa.
13. Wanapenda kutawala mazungumzo.
14. Sangwini ni watu wenye nguvu (Energetic) na mara nyingi hutumia nguvu nyingi badala ya akili nyingi.
Ni watendaji wazuri sana wa kazi, lakini tatizo lao ni kwamba wanatumia nguvu nyingi sana katika utendaji wao kuliko akili. Mara nyingi kazi nyingi zinazohitaji akili zaidi kuliko nguvu huwa zinawashinda. Ndio maana kwenye baadhi ya maofisi wanasababisha migogoro kwasababu kama wamepewa kazi za akili mara nyingi huwa wanashindwa kufikisha matarajio ya wakubwa wao na hapo ndipo migogoro hutokea.
15. Wanapenda kujiunganisha na mambo mbalimbali bila kufikilia kwa undani (Engaging).
Kikundi chochote kinachoanzishwa, au kanisa, au chochote watu wa kwanza kujitokeza na kujiunga huwa ni kundi hili la Sangwini. “Deal” likitokea watu wa kwanza kujiunga ni Sangwini. Mara nyingi huwa wanajiunga hata kama hawajui chochote kuhusu hicho wanachojiunga bora wamesikia tu wanahitajika watu kujiunga wao watajitokeza kwa haraka. Lakini ujue kama jinsi ambamvyo wanajiunga kwa haraka bila hata kufikiri fikiri, ndivyo watakavyo ondoka, baada ya muda mfupi wataondoka bila hata ya kuwa na sababu yoyote ya msingi. Walio wengi wa hawa ndio wanaoongoza kwa kuhama hama makanisa kila kukisha na hata ukiuliza kwanini wanahama hama hawawezi kukupa sabau yeyote ya msingi.
Kukitokea vyama vya kupanda mbegu kidogo na kuvuna sana, hata kama wengine watajiunga lakini Sangwini ndio watakuwa wakwanza kwenda kupanda bila hata kujali wala kujiuliza hayo mavuno yanatokana na nini.
16. Wanapenda Umaalufu na Kujulikana.
Sangwini wanapenda sana kuonekana mbele yaw engine. Wanapenda sana umaarufu wanapenda sana kujulikana na kila mtu na hasa katika maeneo yatakayomletea sifa. Wanapenda sauti zao ndio zisikike, wanapenda sura zao ndio zionekane. Ukitaka uwe rafiki wa Sangwini mpe umaarufu.
17. Ni wabunifu sana. Mara nyingi huwa hawalali njaa. Ni wajasiliamali wazuri sana.
Ukimkuta Sangwini kalala njaa, basi huyo kama ni mjini tunasema wakuja huyo bado anasoma ramani. Sangwini wana uwezo mkubwa sana wa ubunifu wa kufanya vitu mbali mbali hata kama ni vidogo vidogo na wakajiingizia kipato na kusukuma siku. Wanaweza kuongea tu na pesa ikaingia. Wanauwezo wa kubuni vitu ambavyo kwa kawaida usingevizania kuwa vingeweza kuwaingizia kipato.
Siku moja Dar es salaam nilikutana na wanaume wawiwi njiani. Mmoja alikuwa amevaa gauni anajifanya kama ni mwanamke na mwingine amevaa shati na tai ndefu imepita chini ya uvungu wa miguu yake ikatokezea huku nyuma kama mita mbili au tatu hili inaburusa, hiyo tu ilikuwa ni kazi wakipita watu wanacheka wanawapa pesa watoto wanakwenda shule, wanakula wanalipa kodi za nyumba nk.
18. Ni watu wanaopenda urafiki (they are Friendly)
Sangwini anapenda sana marafiki na mambo ya undugu. Wanapenda kutengeneza marafiki kila mara. Kina anapokwenda anapata marafiki wengi tu wapya. Ni hodari sana katika kutembelea ndugu na jamaa na marafiki na kuimarisha mahusiano. Tofauti sana na kundi kama Melankoli, kundi la Melankoli hataki mambo ya ndugu ndugu, au sijui mambo ya vikao vya ukoo au kukutana kutana, hayo ni mambo ya Sangwini. Wewe angalia hapa humu facebook Sangwini anaongoza kwa kuwa na marafiki wengi. Yeyote atakaye muandikia kumuomba urafiki kwa Sangwini hajali kama anamjua au hamjui anadini au hana dini Sangwini kwake ni ku-add tu hayo mabo mengine yatajiseti mbele kwa mbele kwake yeye bora amepata marafiki wengi zaidi. Wakati mtu kama Merankoli mpaka aje kuku-add ujue umepitia michujo ya aina yake kweli. Ni mtu wa watu. Ni mtu wa mahusiano. Nk.
19. Wapo Tayari Wakati Wowote Hawahitaji Maandalizi.
Mara nyingi hata kwenye kazi nyingi za kujitolea Sangwini ndio huwa watu wa kwanza kabisa kujitokeza kwenye jambo lolote. Huwa hawahitaji kujiuliza uliza mara mbili wanaamua hapo hapo na wanakwenda. Ikitangazwa inahitajika watu wajitolee msaada wa damu salaama Sangwine anaweza kujitokeza hapo hapo wakati watu wa makundi mengine wanaweza wakasita kwanza wengine wakasema ngoja kwanza tukajadilianane na wife then tutaleta jibu. Sangwine hana cha kwenda kujadiliana na mke wala mume anafanya hapo hapo. Kama ni mchango na anahela mfukoni atatoa hapo hapo hakuna cha kusubiri.
Tatizo ni kwamba Sangwini hanaga ratiba maalum na hata akiwa nayo hawezi kuisimamia. Kama alikuwa anakwenda Kariakoo ukakutana naye ukamwambia bwana utakwenda siku nyingine huko twendezetu kunduchi unisindikize. Bila kubisha sana atageuza na kuacha shughuli zake na kwenda na wewe kunduchi.
20. Mahali pao pa kazi hapana mpango mzuri pamejaa vitu ovyo ovyo.
Wakati mwingine ukiingia kwenye ofisi ya Sangwine unaweza usipate taabu sana kugundua haiba yake ni ipi kwa haraka sana utagundua. Sangwini wengi wahana mpangilio mzuri katika maendeoe yao. Kama ni ofisini utakuta mafaili yamekaa hovyo hovyo makaratasi kila mahali, yeye mweneywe ili apite anapita kwa kuruka ruka unaweza ukavikiri ni kama jalala la makaratasi kumbe ni ofisi ya Sangwini. Kama ni mama nyumbani Sangwini, akianza kutafuta mwiko usishangae ukaukuta umewekwa juu ya neti.
Ukiingia mlangoni kwake unakutana na sufuria za ugali wa juzi alizoloweka ziko kuanzia mlangoni, viatu juu ya kitanda mito ya makochi iko nyumba ya pili barazani kwa jirani, yaani ilimradi ni vurugu vurugu hakuna mpangilio hakuna utaratibu. Mume mmoja alikuwa ananiambia pasta wala usije ukashangaa kukuta brazia ya mke wangu kwenye friji. Nikacheka sana alikuwa anajaribu kuonyesha jinsi mkewake asivyoweza kupangilia kitu.
Nyumbani kwa Sangwini kama ni nguo za watoto humo humo za baba humo humo za mama humo humo. Ikifika wakati wa kutafuta nguo za kuvaa kutokea wanapanga foleni kama vila wako mnadani kila mtu anachagua za kwake na mbaya zaidi nguo safi na chafu zote zipo kwenye kapu moja utajua hii safi nah ii chafu kwa kuweka puani harufu ndio itakutofautishia chafu na safi.
Kesho nitaendelea na Madhaifu ya Sangwine
Kama umebarikiwa au umejifunza kitu nipe comment kwa kile kilicho kubariki katika somo hili.
Comments