KAZI ZA ROHO MTAKATIFU NDANI YETU





BWANA YESU asifiwe.
Nawasalimu katika jina la BWANA YESU na leo tunajifunza ujumbe muhimu sana uitwao KAZI ZA ROHO MTAKATIFU.
Tunajifunza kazi za ROHO MTAKATIFU kwa sababu MUNGU ni Roho na wanaomwabudu yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli (Yohana 4:24).

Mimi na wewe ndugu ili tumwabudu MUNGU katika njia anayoitaka au njia sahihi na pekee ni kumwabudu katika Roho na kweli.  Kama MUNGU ni Roho na sisi tunatakiwa tuwe watu wa Rohoni na sio mwilini na kwa kutusaidia sasa MUNGU alimtuma ROHO MTAKATIFU ili atusaidie katika kweli yote, yaani atukumbushe, atufundishe,atuonye, atusaidie na atuzingire pande zote ili tutimize kusudi la MUNGU la kumwabudu katika Roho na kweli. Ndugu ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana kwako na kwangu na kama kweli tunataka kumpendeza MUNGU ni lazima tuwe na ROHO MTAKATIFU na pia tumtii yeye siku zote. Ili tuyaishi maisha ya ushindi ni lazima tuongozwe na ROHO MTAKATIFU.
Katika agano la kale manabii walitabiri juu ya kuja kwa ROHO MTAKATIFU mfano Nabii Yoeli aalitabiri katika Yoeli 2:28 na pia Nabii Isaya alitabiri juu ya ROHO MTAKATIFU katika Isaya 44:1-5. Na hata katika agano jipya Yohana mbatizaji alitabiri juu ya ujio wa ROHO MTAKATIFU  na pia BWANA YESU mwenyewe alizungumza juu ya ujio wa ROHO MTAKATIFU. Lakini ndugu kumbuka kuwa ROHO MTAKATIFU alikuwepo tangu milele na hana mwanzo wala mwisho na katika agano la kale alikuwa anafanya kazi kupitia watu wa MUNGU waaminifu.
ROHO MTAKATIFU hutufanya tuwe na tabia ya kumpenda MUNGU 2 Petro 1:1-3, na pia 1Petro 1:3-5.

Tunampenda MUNGU na wanadamu maana MUNGU ni pendo.

 KAZI ZA ROHO MTAKATIFU NDANI YETU.

1:  Hutufanya tumtukuze MUNGU.
              Yohana 16:14
2:  Anatuongoza katika kweli yote.
            Yohana 16:13.
3:   Anatupa uwezo wa kumshuhudia BWANA YESU.(Anatupa ujasiri na ushujaa)   Yohana 15:26, Yoshua 1:5-7.
4:   Hutuombea kwa MUNGU.
           Warumi 8:26.
5:  Anatufundisha. (yeye ni chuo kikuu kuliko vyote duniani)
          Yohana 14:26.
        ROHO MTAKATIFU hufundisha viongozi wote kuanzia Mitume,                                                    Manabii,Maaskofu, Wachungaji, Wainjilisti, Mashemasi na wengine wote.

6:  Hutoa matunda kabisa.
       Wagalatia 5:18-23
  Matunda 9 ya ROHO MTAKATIFU.
I.    UPENDO.
II.   FURAHA.
III.   AMANI.
IV.   UVUMILIVU.
V.    UTUWEMA.
VI.    FADHILI.
VII.   UAMINIFU.
VIII.   UPOLE.
IX.    KIASI.

Hakika kumpata ROHO MTAKATIFU ni kupata uzima maana kama utakuwa ni mwanadamu unayeongozwa na ROHO MTAKATIFU utakuwa na matunda hayo hapo juu. Na kama wanandoa wote wataongozwa na ROHO MTAKATIFU na wakaishi na kuenenda katika matunda hayo 9 hakika amani itatawala daima. Kumbe tunamhitaji sana ROHO WA MUNGU ili tukae salama .
Pia ndugu ROHO MTAKATIFU licha ya kutoa matunda 9 pia hutoa na karama 9 ambazo ni muhimu sana katika kujenga mwili wa KRISTO yaani kanisa. 1 Kor 12:3-11.
Kuna karama 9 za ROHO MTAKATIFU ambazo ni
1: ROHO YA HEKIMA.
2: NENO LA MAARIFA.
3: KARAMA YA IMANI.

4: KARAMA YA UPONYAJI.
5: KARAMA YA MIUJIZA.
6: KARAMA YA UNABII.
7: KUPAMBANUA ROHO.

8: AINA ZA LUGHA.
9: TAFSIRI ZA LUGHA.
MUNGU akubariki sana ndugu kwa kujifunza somo hili muhimu sana na siku nyingine tutaangalia SIFA ZA ROHO MTAKATIFU.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.

Peter Mabula
 Maisha ya ushindi ministry.
pia kama hujaokoka hakikisha unatafuta kanisa la kiroho na uwaeleze ili wakusaidie kumpokea YESU KRISTO na ndipo ROHO MTAKATIFU atakuja  kwako na kukusaidia katika mambo mengi sana hata mambo yako yajayo yeye anajua hivyo atakuambia ili umpendeze MUNGU siku zote. Pia kumbuka kuwa nje na walio katika KRISTO, ROHO MTAKATIFU hawezi kutenda kazi kwako, hivyo kumpata YESU ni Kumpata ROHO MTAKATIFU. AMEN.

Comments

Unknown said…
Barikiwa