Watu
wengi wanajiuliza kwanini wasichana wengi kuolewa imekua tabu?
Research imefanyika kwa wasichana na vijana wa kiume na kupata majibu
sahihi.Imegundulika kuwa matatizo wanasababisha wasichana wenyewe, na
ndio chanzo cha wao kukosa waume wa kuwaoa.
Soma hapa chini sababu za wanawake wengi kukosa wanaume wa kuwaoa kama
ifuatavyo.....
1. MARINGO – Nipale wakati
binti anapokua nakujishtukia kuwa yeye ni mrembo wa ukweli, basi hapoa
ataanza kujisikia kuwa yeye ni yeye kudharau wengine na kujiona babkubwa
na kuwa too much selective, inapotoke kijana kampenda atakapomfata huwa
anamuangalia nakumuona hana hadhi ya kuwa na yeye, itaendelea
hivyoooooo mwisho atakuja kukutana na kijana mtanashati wa ukweli hapo
ndio atajiaminia huyo ndio mwenye hadhi yake kumbe gubegube, mpaka aje
kugundua kashaumizwa anaanza sasa kuumizwa kila mara hapo ataamua sasa
kujishusha na kusarandia vijana wa kawaida, kila atakae date nae anakuta
ni mchumba wa mtu au mume wa mtu au bf wa mtu, hapo ndio tayari
keshakua majeruhi wa mapenzi basi itabidi aishie kuchuna mabuzi fumba na
kufumbua yuko above 30 anaanza kulia nina mkosi ohh nuksi nk.
2. UMALAYA – Ule wakati binti anaanza kuchanua
badala ya kujitunza nakujiheshimu yeye ndio anatumia nafasi hiyo
kuuchezea mwili wake kila mwanaume anayemtongoza anamkubali mwisho
anajikuta ana maboyfriend zaidi ya mmoja, hapo anaanza kuangalia sasa
maslahi na sio upendo wa dhati anajikuta kaingia kwenye wrong choice
basi ataendelea kusakanyia mwengine na mwengine na mwengine ili akutane
na right choice hapo kuna mabuzi kibao kuna waume za watu na vijana
matapeli wote anabambana nao mwisho anashtukia yuko above 30 ana anza
kulia ohh na mkosi sijui nuksi nk.
3.
MAJINI MAHABA – Baadhi ya wasichana wana majini mahaba kwahiyo kuolewa
kwao imeshakua ni tabu anaweza apate mchumba afe au mwanaume abadilike
tabia nakumchukia au mwanaume aanze kuwa Malaya na kushindwa kumvumilia
hatimaye wanaachana mauzauza yanakuwa kibao kwenye mapenzi yake mwisho
anajishtukia yuko above 30 anajiona ana mkosi na nuksi.(Lakini kwa maombezi kupitia jina la YESU KRISTO utafunguliwa kutoka kwenye roho hii ya shetani. kimbilia kanisani na utapona)
4.
MARAFIKI WABAYA – Msichana anaweza kuwa haolewi kumbe marafiki alionao
sio wema kwake, ukipata mchumba tayari umeshaenda kumweleza shosti wako
au mashosti zako, bila wewe kujua wanampeperusha, watakuzunguka
,watatembea nae, watamtega, watakuongelea vibaya, watakuloga, watamloga,
watakuharibia mpaka utaachwa kila mara usipokua mjanja ukashtuka ndio
hivyo uanajikuta uko abave 30 unaanza kulia ohh nina mkosi sijui nuksi
nk.
Mpaka hapo nina amini kwa wewe msichana ambaye huolewi kuna fungu lako
moja kati ya hayo hapo juu, sasa chakufanya jitambue na ujipange upya
kama ushapita above 30 usihofu sana hata miaka 60 wanaolewa bado.
MUNGU awasaidie mabinti na kumbuka mme/ mke mwema anatoka kwa MUNGU.
Hivyo maombi kwa ajili ya mke/mme lazima yafanyike mapema ili MUNGU
amlete kwako yule ambaye madhaifu yako atayaona kama moja ya mambo mema
zaidi kwako. MUNGU akupe macho ya rohoni ili uutambue ukuu wake. MUNGU
awabariki na amani ya KRISTO YESU iamue mioyoni mwenu.
Comments