MAMBO YA KUFANYA ILI KUUDHIBITI MOYO.

 Na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira


Moyo siku zote una hila ni muhimu kujiuliza MOYONI Mwako UNAWAZA Nini? Unamwazia nini MWENZIO, MUMEO, MKEO, au RAFIKI YAKO? Moyo Umepata MAJERAHA Kiasi gani?, KINYWA Chako kinatoa Maneno gani? UNATAFAKARI nini moyoni mwako? Kwa kuwa TUTAHUKUMIWA Kulingana na TULIVYOTUMIA MOYO Wetu, ni MUHIMU kama Wana wa MUNGU Kuelewa vilivyo MOYO WAKO UNAANDAA Nini ili BWANA AKUJIBU. Biblia Inatuambia kuwa “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu lakini jibu la ulimi latoka kwa MUNGU” (Mithali 16:1). Ili uweze kuwa na maandalio ya MUNGU ndani yako yakupasa useme “Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mwokozi wangu” (Zaburi 19:14). ELEWA kuwa Moyo unao MATAKWA yake, Vile vile MUNGU Naye ANAYO MATAKWA YAKE. Kwa hiyo kutokana na hali ya Moyo wako, UNAWEZA KUFUTA KILA KITU CHEMA Alichoandaa MUNGU kwa ajili Yako.

Moyo unabidi ULINDWE ili uwe na UZIMA Sawasawa na Biblia inavyosema. Hatua ya kwanza ni KUKUBALI kuwa Hauko Mkamilifu bali UNAHITAJI NEEMA YA MUNGU ili IKUWEZESHE Kila Iitwapo leo. Bainisha kwa UAMINIFU MATATIZO YA WAZI Na YA SIRI Ndani ya MOYO WAKO, Ukiangalia jinsi UNAVYOWAZA, UNAVYOAMUA na UNAVYONENA. Angalia Majeraha na Maumivu Uliyo nayo moyoni mwako. USIPOTEZE MUDA Kuwaza watu wanasema nini juu yako wala USIKUBALI KUKAA na Moyo ULIOJERUHIWA au KUINAMA.

Sasa JIPELEKE mbele za MUUMBA WAKO UJIELEZE Waziwazi. TUBU kwa Kweli halafu Mpe YESU moyo wako, aweze KUUSAFISHA Kwa damu yake ili AUFANYE KUWA MPYA.''

Comments