MASHAMBULIZI KATIKA NDOTO


Lengo Kuu: Kujua Jinsi gani wachawi hupambana na wanadamu kwenye ndoto
Lengo Mahususi: Tunawezaje kuwashinda Mashambulio haya katika ndoto.

Tafiti zinaonesha kuwa, Karibu kila aliyeuawa na nguvu ya wachawi aliota kwa namna moja au nyingine. Ndoto hizo ni pamoja na kuota unapigwa risasi,unagombana na mtu unayemjua au usiyemjua anaweza akawa, jirani, mme,mke, mtoto n.k.
Ndoto nyingine ni pamoja na zile za kufukuzwa na vichaa, kukimbizwa na wanyama wakali na hatimaye kukupa hofu sana. Hizo ni roho ambazo wachawi huzitumia kujaribu imani yako na kupitia ndoto hizo hukushambulia sana. Aidha, inakupasa ujue kuwa endapo utakamatwa na vichaa hao wanaokukimbiza, au kama ukianguka wakati unakimbizwa, hiyo ni dalili ya kushindwa kwako. Unapaswa kuomba Mungu sana na Kujifunika kwa damu ya YESU.
Pia, kama unaota unaongea na watu waliokufa huku wakisema kuwa ni rafiki zako, kutokewa na sauti za watu waliokufa hususani unapokuwa peke yako hata kama ni mchana, jua hiyo ni mbinu ya kipepo kwa kuwa unatumiwa mizimu ili ije kukuita na kukutambulisha kuzimuni. Ita jina la Yesu kwa kumaanisha ili ujiepushe na nguvu hizo zinazokufuatilia.
Ndoto nyingine zinazotumiwa ni sawa na zile za kuota uko porini peke yako, kuota uko kwenye giza nene linalokupa hofu. Pia, kuota umeumwa na wadudu wakali kama siafu, nge, tandu,nyuki, manyigu, nyoka na mbwa ni dalili mbaya hasa kwa wajawazito kwani huashiria kuchukuliwa kwa mtoto aliyeko tumboni, hii husababisha mimba kuharibika zaidi karibu na kujifungua. Pia ndoto zinazokuja zikikuonesha kuwa unajifungua alafu anaepokea mtoto humfaham, au pengine unaona mikono tu ikipokea mtoto, ni ndoto za kipepo ambazo zinachukua mtoto wako; ndoto hizi zinaweza kupelekea mtoto kufia tumboni, na hata wakati mwingine mama kupata kifafa cha uzazi ambacho kinaweza kusababisha kifo chake. Jambo la msingi hapa, ni kukemea nguvu zote za giza zilizokuzunguka, huku ukiukabidhi ujauzito wako kwa Yesu ili aulinde wala adui asiweze kuuharibu. Kwa kufanya maombi haya, unaweza kuzuwia kifo hiki, unaweza kuzuwia upasuaji wakati wa kujifungua na unaweza kunusulu maisha ya mama na mtoto, japo mara nyingi mtoto. Kufanya hivi kunakupa usalama kutoka na ahadi ya neno la Mungu ya kuwa “...kila atakayeliita jina la BWANA ataokoka” (Warumi 10:13). Kuoka hapa maana yake ni Kunusurika, kuponea chupu chupu. Unapaswa kujua kuwa jina la Yesu lina nguvu sana na lina mamlaka kamili juu ya vitu vyote duniani na mbinguni,vinavyoonekana na visivyoonekana, hivyo kwa kufanya hivyo utakuwa umeahirisha msiba wako. “Kwa kuwa katika yeye, vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni, na vilivyo juu ya nchi vinavyoonekana na visivyoonekana ikiwa ni vitu vya enzi au malaika, vyote viliumbwa kwa njia yake na kwaajili yake.” (Wakolosai 1:16,)” ...Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na vya nchi kavu....”(Wafilipi 2:9-11)
Hatahivyo, pamoja na nguvu iliyoko kwenye jina la Yesu na mamlaka yote, unapaswa kujua kuwa, unapaswa kuishika haki yote ili kuweza kupata msaada huu yaani kuwa na imani na kusihi katika hali ya kumpendeza Mungu. Pepo wanamjua Yesu, na wanamwogopa, ila hawashituliwi na anayetumia jina hilo kama hajashika haki kamili ya jina la Yesu.(Matendo 19:13-16) “baadhi ya wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga mapepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na mapepo....yule pepo mchafu akawajibu, akawambia, Yesu tunamjua na Paulo tunamfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu mwenye pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda hata wakatoka mbio ili hali wa uchi na kujeruhiwa.”
Ninachotaka kukwambia hapa ni kuwa, unapaswa utambulike katika ulimwengu wa roho kwanza na hapo ndipo Jina la Yesu litakupa ushindi, na ukisomeka kwa kuwa na jina la Yesu, kila utakacho kiamuru kitakutii, kutokana na mamlaka unayotumia ambalo ni jina la Yesu ambalo kila kilichoumbwa kinatii na kutetemeka mbele yake. Unapaswa kujua kuwa, kulitaja jina la Yesu bila kutambulika katika ulimwengu wa roho ni sawa na kuwa na simu isiyo na chaji japo kweli salio linatosha, ila huwezi kupiga simu wala kutuma ujumbe wowote, kwasababu hauko hewani; hivyo basi unapaswa kuwa kwenye mtandao na malaika wa mbinguni ili kuambatana na jina la Yesu Kristo. Na hii ndiyo maana Yesu mwenyewe anasema “ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote, nanyi mtapewa” (Yohana 15:7). Ndugu yangu, naomba ni kwambie kuwa maombi yako daima, yapeleke mbele za Yesu mwenyewe, hapo ndipo utakapojibiwa, naomba nikwambie kitu kimoja, epuka mafundisho ya uongo ambayo maombi yanapitia watu waliokufa eti kwa kuwa ni watatifu, mitume au manabii wa zamani, bibilia inasema hayo ni machukizo mbele za Mungu, wala Mungu hawezi kuyajibu, kwa kuwa anasema hayuko radhi na wapumbavu, ebu omba kupitia Jina la Yesu kwa kuwa ndiyo anuani tuliyopewa. Kuomba kupitia wafu au watu wengine kama Paulo, Isaya, Bikra Maria na Watakatifu wengine, siyo njia sahihi, ni sawa na mtu unampigia simu halafu, unakosea namba, kimsingi hutampata, nawaomba mbadirike, liangalie neno la Mungu linavyosema, yapuuze mafundisho ya upotovu. Hayatakusaidia lolote.
Kwa upande mwingine, unapoota unaumwa na mbwa au nyoka, au kukimbizwa na wanyama hata wakakuangusha, humaanisha kuwa uko dhaifu kiroho. Pia, unaweza kuota majitu yenye sura zisizo tambulika sahihi na pengine kuona vivuli vinakukaribia au vinyago, hii ni hatari sana kwani ni ishara ya kuwa adui yuko karibu yako, anaweza akawa rafiki au hata ndugu na amekushinda kumtambua, hivyo amekudhoofisha kiimani na karibu atakuangamiza. Ndoto hizo pamoja na zile zakuota unaliwa na wanyama mwitu kama vile simba, chui na mbwa mwitu, au kuota unachukuliwa hewani, huweza kusababisha mtu kuvurugika akili na hata kuehuka. Hii ni hatari sana, kwani zinatumika sana kuangamiza watu kupitia njia hii. Pia, mara nyingi huweza kuota umetoka huko unatembea na watu ambao huwajui, aghalabu huongea vitu/lugha ambavyo huijui, na wakati mwingine hujisikia unagandamizwa chini, ukijaribu kupiga kelele au kuamka unashindwa, zote hizi ni dalili za kulegea kiroho na huweza kukupelekea mashambulizi makubwa ambayo hukuotesha ndoto chafu huku ukiwa unalishwa vitu mara nyingi nyama, ukifanya tendo la ndoa na watu usiowajua. Hii huufanya mwili kuwa najisi na kuibomoa madhabahu ya roho mtakatifu anayekaa ndani yako, hivyo mapepo kupata nafasi. La msingi, chukua hatua ya kufanya maombi ya muda mrefu usiku huo, na anza maombi makavu yaani kufunga bila kula wala kunywa walau masaa kumi na mawili. Fanya hivyo mara nyingi zaidi, na tenga muda wa kusoma neno la Mungu, huku ukilitafakari kwa kina. Aidha, jenga mazowea ya kuamka usiku na kuomba na kukemea nguvu zote za giza, huku ukiita ulinzi wa malaika wa Mungu.
Kumbuka, “....kushinda kwetu sisi si juu ya damu na nyama;bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili , juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” Efeso 6:12. Pia, Yesu mwenyewe anasema, “Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui wala hakuna kitu cha kuwadhuru” Luka 10:19.
Mungu awabariki na kuwapa Ulinzi daima. Akupeni uwezo wa kuizishinda njia zote za adui, na mipango yote ya kipepo iwe chini ya nyayo zako. Amen

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7 (57/84) 464 141/ 12 909 021.
Au Email sos.sesi@yahoo.com / newelshaddai@gmail.com

Tunakushauri, utembelee kanisa la kiroho lililo jirani yako, kwaajili ya mafundisho zaidi na Ushirika. (Kumbukumbu la Torati 28:6).

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7 (57/84) 464 141/ 12 909 021.

Comments

Anonymous said…
Shalom!

Nashukuru kwa article/makala hii...ni njema na imenibariki. Ingawa naomba kujua tafsiri ya ndoto hizi 2

1. Mke wangu aliona/aliota mjusi akiwa pembeni ya kitanda karibu na ninapoweka kichwa...mara mbili katika usiku mmoja. Na kwa maelezo yake, alipowasha taa ya simu mjusi alikimbia...ingawa mimi sikuona chochote, je hii ina maana gani ??

2. pia mke wangu amekuwa akilalamika kuwa huwa anaota kuna mtu ambaye amejifunika nguo nyeusi ambaye huwa anajaribu kumkaba. Na nimekuwa nikimuona mara kwa mara akiwa anaweweseka....kama vile amashindana na kitu. Je, hiyo ina maana gani ?

Ahsante & Barikiwa.