''MOYO ULIOMBATANA NA MUNGU

  Na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira


MOYO Uliombatana na MUNGU unakuwa na AKILI NZURI, MAARIFA na UJUZI na IMANI yake ni Kubwa kwa kuwa UMEHUISHWA. Unakuwa MWEUPE (Daniel 1:17, Yakobo 1:5 -7, Matendo 7:22), Mtu mwenye Moyo Safi huwa Mahiri sana na Mwangalifu katika KUENENDA na KUTENDA katika HEKIMA YA MUNGU. Mtu wa Namna hiyo mtazamo wake ni wa KUJIAMINISHA kuwa Agizo la KUFANIKIWA ni AMRI YA MUNGU na ya Kuwa KUKIRI na KULITAFAKARI NENO ndipo Hukaa MOYONI, Vinginevyo hilo NENO Huondoka kwake. Tena ana Hali ya KUFANIKIWA KATIKA KILA JAMBO Afanyalo, KIROHO na KIMWILI Kwa kuwa Anapata KIBALI KWA MUNGU. Hali hiyo huleta KICHEKO, FURAHA, MEMA na UZIMA WA MILELE Kwa Mtu huyo. Aidha HEKIMA YA MUNGU huwa ndani yake na hata ANAPOONYWA Jambo Fulani Kuhusiana na KOSA Alilolifanya HUONYESHA TABIA ZIFUATAZO:-
- Hutokwa na MACHOZI ya KUJUTIA Kile kilichotendeka kutokana na Makosa yake,
- HUTAFAKARI ni Wapi Amekosea,
- Hufikia TOBA YA KWELI,
- HUBADILIKA Tabia yake.

Endapo Utapata Fursa ya KUONYESHWA UDHAIFU WAKO katika Jambo au Maneno Uliyoyasema, ANGALIA JINSI UNAVYOJISIKIA NDANI. Hiyo ndiyo DALILI YA MOYO Uliyonayo. Biblia inatujulisha kuwa, “Usimkaripie mwenye dharau, Asije akakuchukia; mkaripie mwenye Hekima, naye Atakupenda” (Mithali 9:8). Tena inatuasa ya kuwa mtu mwenye kusikia maagizo ya MUNGU HUFANIKIWA na KUITWA Mwenye AKILI. “Basi kila asikiae haya Maneno yangu, na Kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye Akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba” (Mathayo 7:24)''

Comments