MSINGI THABITI WA BARAKA ZETU



Na mtumishi wa MUNGU Peter Michael Mabula

{ 1 wakorintho 3:11-14''Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. } 
Ndugu msingi wa baraka zetu ni BWANA YESU maana hakuna msingi mwingine
 -kumbe  kuna  Baraka  nyingi hasa  zinatoka  na  mikono  lakini  hatujishugulishi  {zaburi 24:4-5 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.  Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. } 
 kumbe  kila  Baraka  ina  kanuni  yake mfano  wanafunzi  wa YESU walikuwa  wavuvi  hata  uvuvi  una  kanuni zake  hivyo  lazima  ufahamu  kanuni  hata  Baraka  zina  kanuni  zake  mfano  kusonga  ugali  lazima  ujue  kanuni 

-Waisraeli  waliambiwa  watapewa nchi  ijayo  maziwa  na asali  {kutoka  3:8}

-Niwaokoe  kwa  mikono  ya  wamisri

-Farao  aliona  mikono  ya  musa  kumbe ndani ya mkono wa Musa kulikuwa na  mkono wa MUNGU {kutoka  3:20 Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda. }

 -Nami  nita unyosha  mkono   wangu  na  kupiga  misri  lakini  MUNGU alitumia  mikono   ya  Musa 

-kumbe  kuna   mikono  inayo  leta  madeni  tabu  na  mengi  na  leo tunashughulika  na  mikono 

- Lazima   tujue  mkono  wa  MUNGU uletao  Baraka 

-waisrael  walipoanza  safari  kuondoka  utumwani   misri njiani  walipata  vipingamizi  lakini  haikuzuia  agizo  la  MUNGU kwamba  kuna  nchi  ya  maziwa   na asali 

-Kanuni  ya  jangwani  ni  tofauti  na  kaanani  {kutoka  4:} BWANA  akamwambia  Musa  akazifanya  ajabu  zote  alizozitia MUNGU  kwenye   mikono  ya  Musa 

Kumbe  tuna  ona  Baraka  kuajiliwa  hivyo  lazima utumie  mikono  yako  ili  kuzihilisha  Baraka  za  BWANA  {kumbu 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. }

-Bali  utamkumbuka  BWANA MUNGU wako  maana  ndiye  akupaye  nguvu  za kupata  utajili, ili  imani agano  lake {mithali  8:18 Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. } 

- utajili  heshima  ziko kwangu  naamu  utajili udumu  na  haki 

Adamu  aliambiwa  zaeni  ili muongezeke  kwa  hiyo lazima maze  ili  uongezeke  pasipo  kuzaliwa huwezi  kuongezeka

-Baada ya  kutoka  kwenye safari  muhimu   akaaza  kuwa  mkulima  {kumb  28:1-6} {mithali  10:4}  {mithali  10 :22} Baraka  hutajilisha  wala hachanganyiki  kanuni  nayo. 
Ndugu ni muhimu kufanya kazi na MUNGU atakubariki kutokea kwenye hiyohiyo kazi hata kama ni ndogo kiasi gani.
MUNGU awabariki sana
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula
      Huduma ya Maisha ya ushindi  


Comments