MTOTO AFUFUKA KIGOMA BAADA YA MAOMBEZI



Mama Mzazi wa Dickson, Happiness Joseph alijikuta akibubujikwa na machozi ya furaha alipompokea mtoto wake akiwa hai baada ya maombi ya kumfufua kutoka kwa Mch. Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi la Kigoma, Paul Joshua.

Mama huyo alifiwa na mtoto wake jioni na bila kujali watu wanasema nini aliamua kumkimbizia Kanisani, likiwa ndilo tumaini lake la Mwisho. Kam vile Yesu Kristo alivyo mfufua Kijana katika lango la Naini vivyohivyo alimtumia Mch. Paul na watendakazi wa Ufufuo na Uzima - Kigoma kumrudisha Dickson katika uhai wake.

Pichani ni mtoto Dickson akiwa amekufa, wakati wa maombezi na ushuhuda baada ya kufufuka.

"Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina yeye."

Comments