MUNGU ATAKAVYOKUSHINDIA,HATA SHETANI ATASTAAJABU.

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.


Ndipo Nebukadreza akastaajabu,akainuka kwaharaka;akanena,akawambia mawaziri wake,Je!hatukutupa watu watatu,hali wamefungwa,katikati ya moto?Wakamjibu,wakmwambia mfalme,kweliEe mfalme.

Akajibu, akasema,Tazama, mimi naona watu wanne,naowamefunguliwa,nao wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara;na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.
(Daniel 3:24&25).

Kama Nebukadreza,alivyostaajabu na baraza lake lote vile Meshack, Shadrack na Abednego Mungu alivyowatetea dhidi ya hukumu yake(Daniel 3:20) na kumdhirishia kuwa Mungu wao anaweza kuwatetea hakika kama walivyotumaini tangu awali((Daniel3:17); ndivyo hivyo jaribu lako litakavyostaajabu, utakapolishinda bila kumwasi Mungu wako.

Ndugu yangu, nakuhakikishia, ugumba utashangaa utakapo pata mtoto,hilo pepo la kuzuwia mafanikio yako katika biashara yako,katika ndoa, katika masomo litakavyostaajabu. Pepo la magonjwa litastaajabu uwezo wa Mungu aliye hai, Mungu aliye hai (Daniel 3:26)wa Shadrack Meshack na Abednego na kuweka mikono juu, endapo utalishinda kwa waminifu wote.

Hakika nakwambia, Usitishiwe na misiba,wala magonjwa wala hasara,Mungu anampango mzuri juu yako, usidanganywe na vinjonjo vya shetani.Mungu anaenda kukutetea na kukushindai wala hutakuwa kama ulivyo kwa Jina la Yesu.

by  Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Comments