MWENYE HAKI NI NANI NA ANAPONYWA WAKATI GANI?

 Na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).


"Zaburi 34:19 “Mateso ya mwenye haki ni mengi; lakini BWANA humponya nayo yote”

Zaburi 107: 19-20 "Wakamlilia BWANA katika dhiki zao akawaponya na shida zao. Hulituma Neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao”.

Hili ni Neno la MUNGU na limegawanywa katika mazingira yafuatayo:-
- Neno la MUNGU ni Moto
- Neno la MUNGU ni Upanga
- Neno la MUNGU lina NGUVU za Kuokoa
- Neno la MUNGU lina Uwezo wa Kutimiza lilichotumwa maana Neno linasema, “Ninalituma Neno langu na halitanirudia bure mpaka limetimiza kile lilichotumwa”

MWENYE HAKI NI NANI NA ANAPONYWA WAKATI GANI?

Yeyote ambaye amedhamiria moyoni mwake KUMCHA MUNGU wa kweli, huyo ndiye anaitwa MWENYE HAKI; haijalishi dhambi gani aliyoifanya; haijalishi makosa aliyonayo lakini kama AMEDHAMIRIA moyo mwake KUMWANDAMA MUNGU WA KWELI.

Mahali pengine Biblia inasema, MUNGU wetu ni KIMBILIO, Wenye HAKI Wakikimbilia Hukaa salama. Mwenye Haki HUMWABUDU MUNGU WA KWELI.

Eneo lingine Biblia inatumabia, “Hakuna mwenye Haki, wote wametenda dhambi na kupungukiwa na Utukufu wa MUNGU”, lakini wale MUNGU anasema, Zaburi 16:3, “Watakatifu walioko duniani ndio Walio bora, Hao ninaopendezwa nao. (Wale waliaminio Neno LAKE”, ndio anaowatafuta.)

Kuna watu wako duniani, ni wenye dhambi lakini anawapa Haki KATIKA YULE ALIYEWAOKOA, YULE ALIYEWAFILIA. Yeye Haangalii dhambi zake bali NIA YAKE na LENGO LAKE KUHUSU MUNGU. Lengo lake ni Nini?
- Lengo la KUMWABUDU YEYE
- Lengo la KUMWISHIA YEYE
- Lengo la KUMCHA MUNGU
- Lengo la KUMTUMAINI YEYE
- Lengo la KUTAKA YEYE Kwa Wema Wake ANIOKOE
- Lengo la kutaka YEYE kwa HURUMA YAKE ANIHURUMIE, ANIPE REHEMA.

Sasa MUNGU Anapoona nia ya MOYO WAKO ni kutaka KWAKE AKUTENDEE JAMBO, Ndipo ANAPOKUITA WEWE NI MWENYE HAKI.

(Maneno haya Matakatifu, Yenye HEKIMA na UFAHAMU Yataendelea...)

"Mwana wa MUNGU huu ni wakati wako wa KUTOKA, USIKUBALI Tena, Ni wakati wako Mwana wa MUNGU KUTOKA, ni wakati WAKO."

BWANA Akakuridhie.”

Comments