![]() |
Msafara wa Mapokezi ya Mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola kutoka Airport Mwanza |
Mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola umewasili Mwanza tayari kwa taratibu zingine kufuatwa ikiwa ni kuwapa nafasi wakazi wa Mwanza na Mikoa jirani kutoa heshima zao za Mwisho kabla ya Mazishi yatakayofanyika siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa maelezo ya awali, Mwili wa
Askofu Dr. Mosses Kulola utaagwa Siku ya Jumanne katika Uwanja na CCM
Kirumba na Mazishi yatafanyika Siku ya Jumatano katika Kanisa la EAGT
Bugando.
Endelea kutembelea Mtandao huu, na
tutakufahamisha kila linalojiri Mkoani Mwanza kuhusiana na Msiba huu wa
Baba/Babu yetu mpendwa Askofu Dr. Mosses Kulola. Picha za Mapokezi ya
Mwili wa Marehemu tutaziweka muda mfupi ujao.
chanzo:gospel news media
Comments