NANI KAKWAMBIA MUNGU ANATAKA WALIOKOSA PA KWENDA?

Na Mwl Sospeter Simon Ndabagoye


MKUMBUKE MUUMBA WAKO SIKU ZA UJANA WAKO.
Ujana,ni umri ambao mwanadam huishi akiwa katikati ya utoto na utu uzima au uzee. Kipindi hiki cha kiukuaji, huhusisha shughuli nyingi na mabadiriko kadha wa kadha katika maumbile,uwezo wa nguvu na hata akili n.k. Hata, hivyo, kipindi hiki,pamoja na vile vingine, vimewekwa kwa mpango kamili wa Mungu na kwa muda maalum, unaopimika kwaajili ya utukufu wake mwenyewe.

Biblia inasema katika Ayubu 14:1-2“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe”
Rafiki! Leo tunatafakari juu ya UA, wote tunajua kuwa UA LIKICHANUA KINACHOFUATA NI KUNYAUKA, na Jambo la kuvutia zaidi ni kuona linavyopendeza na kuvutia, mbali na wanadamu kupenda MAUA, hata wadudu pia utakuta wamejazana.

TAFAKARI.
Ebu fikiria kwa kina, ua linapochanua, wakati mwingine huwa halina harufu, na hata likiwa na harufu huwa haivutii. Lakini,mara linpokuwa limechanua
linapochanua,hutoa harufu nzuri kama manukato mazuri, na hata harufu yake huwa kama marashi mazuri na ya kupendeza, kitendo hiki,hupelekea hata watu,wanyama na wadudu kutamani uzuri huu, na kuamua kuyafanya kuwa rafiki, ndiyo maana, huyapamba majumbani, na pengine wadudu hufurahia harufu ya manukato katika kutengenezea chakula chao na watoto wao. Lakini,ua halitadumu katika hali hiyo tu,bali litakomaa,litasinyaa na pengine hudondoka na kuoza,huku likiacha utomvu ukidondoka,unaotoka kwenye jeraha la kondo la ua na hatimaye kuweka tunda au kovu la kudumu. Hii ina maana kuwa, hitimisho la ua liko kwenye kuchanua kwake. Kwa kuwa,kuchanua kwake, ni mwendelezo wa hatua zinazofuata,zinazopelekea kufa kwake. Huwa hasara na huzuni kwa wadudu,ndege, wanyama na hata binadamu,anapokuta ua limenyauka, ila huzuni hiyo si zaidi ya maumivu upatao mti ule uliopoteza sehemu yake yenyewe, na kupelekea jeraha lisilo na mwisho. Kwa ufupi,kudondoka kwa ua, ni mwanzo wa ulemavu wa mti husika.

Hata sisi, maisha yetu wanadamu, yamefichwa katika mfumo wa ua, unapochanua hupendeza, na huvutia kwa kila anaekuona. Kwa nguvu na sauti,ubabe na sura,huvitisha vyote na kukuogopa, lakini mwisho huwa ni kuvuka hatua hiyo,na kubaki Historia kichwani. Aidha, huwa simanzi kubwa, ujana unapopotea bila mannufaa kwako mwenyewe na jamii kwa ujumla. Humsikitisha kila mtu, hata asiyekujua, anapopata taarifa juu ya habari zako,endapo hutokea huku,hujakamilisha malengo yako.

Maumivu haya, wapatayo wanadamu, hayafikii hata nukta ya yale apatayo aliyekuumba,anapoona muda wako wa kuishi unaisha kabla hujafanya jambo lolote kwake.Huumia sana, anapoona nguvu zako,akili zako, mali zako na hata wewe mweyewe,unaishia kumtukuza shetani. Utumia mtaji wa uzuri wako kufanya umalaya,pesa zako kunyanyasa watu,kufanya maasi, unatumia wadhifa wako,kunyanyasa watu, unatumia elimu yako kuwaibia watu; badala utumie kwaajili ya utukufu wake.
Ndugu, kila mwanadamu alipo, Mungu amempa kitu maalum kwajili ya kumtumikia (Warumi 12:6-8) na kwajili ya utukufu wake, hivyo ni vyema,utumie kwaajili yake na kwa utukufu wake.

Ndugu yangu, kama tulivyokwishaona "Mwisho wa UA kuchanua ni kunyauka" na wala haikawii sana, ni muda mdogo tu, ua huchanua, na kunyauka ghafla; wadudu, hutumia wakati vizuri,ua lingali limenawili, hata mpambaji, huchuma ua,lingali limechanua vizuri, hakuana atakaye penda ua likisha nyauka na kuakauka, hata wadudu, hawalitamani,mpambaji tu, akilikuta kwake limevunda, hataki hata kulinusa, hulichukua tena kwa kijiti na kulitupa kwenye shimo la taka,ambapo hungojea taka nyingine ili viteketezwe kwa moto. Na huo, huwa ndiyo mwisho wa ua, lililo kuwa zuri lilipochanua na kupendeza.

Hat sisi, Mungu anatutaka,tumtumikie, tukiwa vijana, tukiwa na nguvu tena tumtumikie tukiwa tumesoma, tukiwa tunapendeza, Mungu, amewaumba mkiwa ma Handsomeboys ili mmtumikie, wala hajawaumba ninyi warembo kwaajili ya ukahaba na umalaya wenu.

Mungu si mjinga kukupa mwili na nguvu zote hizo ili ukazitumie kwa ujambazi na unyang'anyi. Wala hajakupa akili kwaajili ya wizi na ufisadi. Hata hiyo ofisi ulikalia,hajakupa kwaajili ya kuitumia kwaajili ya tamaa zako za mwili. Huyo Sekretari mzuri, hayuko hapo kwaajili ya tamaa zako za mwili; na wewe sekretari, huyo bosi wako, jua yuko hapo kwa kuwa Bwana kamweka, si kwaajili ya tamaa zako mbaya. Tumia muda wako na nafasi yako vizuri. Tumia kila ulichonacho kwaajili ya utukufu wa Mungu.

Usidnganywe na hao waharibifu, kama maua yanavyo haribiwa haraka na wadudu. Utakuta mtu anavuta bangi, anashindilia unga, umalaya,wizi,ulevi wa kila namna,kila siku ugomvi usiokwisha, mpaka mwili wote unachakaa,unakuta mtu hana meno wala kucha kwaajili ya kipigo. Umeuchosha mwili. Mtu mzima na anafamilia, halafu ni shoga, ni msagaji, amechoka, amechakaa, hafai hata kumtazama tu, ameharibiwa,karibu anadondoka, na akishadondoka lazima asinyae na mwisho wake ni shimo la takatala na kupigwa kiberiti.
Ndugu yangu, usikubali sigara ikuharibie maisha yako,wala uongo ukutoe kwenye kusudi la Mungu wewe kuwepo duniani. Kama lilivyo shimo la taka, kwaajili ya taka, hata jehanamu ipo kwajili ya shetana. Mungu hakuweka jehanamu kwaajili ya binadamu; bali shetani huwaharibu watu,ili apate wa kwenda nao. Jisalimishe leo, ukoke,uepuke moto huo.
Mungu, anataka hiyo sauti yako imwimbie, uikomboe kutoka nyimbo za kipepo,ikaimbe kanisani. Hiyo pesa yako, ikapeleke injili vijijini,ikajenge kanisa huko ambapo injili haijafika. Mungu anatamani sana, aone ofisi yako, imefanyika kuwa kituo bora cha huduma na haki.
Usikubali kutapeliwa na shetani, huyu mdudu asiye na meno. Using'anga'anie dhambi,njoo kwa Yesu upone.

Kuna wengine, wanadai kuwa "wanatesa" kumtumikia Mungu ni mpaka uzeeke!!! Hayo ni mawazo yaliyotapeliwa.Kumbuka, Mungu anaujua ujana na waheshimu vijana kama nguvu kazi, ndiyo maana anawataka vijana wamtumikie. Na hapo ndipo anaposema, "amelaaniwa yeye atendaye kazi ya Bwana kwa ulegevu" hii ina maana kuwa, Mungu anakutaka ukiwa na ujana wako na nguvu zako, ukiwa na elimu yako,ukiwa na pesa yako na hata hilo gari lako pia analitaka, na hiyo nyumba yako.

Unapaswa kujua kuwa, Mungu, hataweza kukumbuka kama,wewe hutajisahau kwanza. Kumbuka, hata Ibrahimu, alimpendeza Mungu na kukubarika mbele zake alipojisahau kuwa Isaka ndiye mrithi wake, na kukubali kumtoa sadaka (Mwanzo 22). Hata leo, Mungu anataka umtumikie katika hiyo hali unayojitamani wewe mwenyewe, Mungu hana haja na huo uzee wako wala Mungu hajafirisika eti,umtumikie na hizo cheji zako eti ni sadaka, wala kumwimbia kwa kuwa umekosa cha kufanya,wala kujifanya kumtumikia eti kwa kuwa umekosa kazi,kumbuka "MUNGU si mnafiki,na tena hayuko radhi na wapumbavu" achana na hayo mawazo finyu,kuwa Mungu anatumikiwa na masalia,waliokosa pakwenda. "MUNGU, hadhihakiwi hata siku moja"
Kila mwenye pumzi ya uhai wa Mungu (neno) anapaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu daima.

Mungu atusaidie wote.
Mwl. SOSPETER SIMON

Comments