Padre wa kanisa katoliki Zanzibar Anselmo Mwan’gamba amwagiwa tindikali

Padre Ancelmo Mwang'amba baada ya kumwagiwa Tindikali
Kwa mujibu wa WAPO Radio FM kupitia kipindi chake cha Yaliyotokea jioni hii, Padri Anselmo Joseph Mwan'gata wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, mkoa wa mjini magharibi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, alikuwa internet café majira ya saa tisa alasiri maeneno ya Mlandege.



Kwa mujibu wa kamanda wa Jeshi la Polisi mjini Magharibi, Mkaadanu Hassan Mkaadanu, Padri huyo alipigiwa simu, na alipokuwa akitoka nje ili kuisikiliza vema simu, hapo ndipo tukio likatokea, ambao haijajulikana kama ni mtu au kundi la watu lililofanya tukio hilo.



Taarifa za hivi sasa zinaeleza kuwa Padri Mwan'gata amelazwa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja, wodi ya Mapinduzi mpya, ambayo ni wodi maalum kwa ajili ya viongozi.



Gospel Kitaa imeelezwa kuwa Padri huyo amefanya kazi kwa muda wa zaidi ya miaka 35 huko Zanzibar, ambapo baada ya taarifa hizi kupatikana, askofu mkuu wa kanisa katoliki Zanzibar, Agustino Shao ameelezwa kujifungia kuanzia muda huo na kuendelea kuwepo hadi muda huu ambapo ripota wa WAPO Radio FM, ameeleza.



Kwa hivi sasa taharuki ni kila mahali, hakuna kinachoeleweka, wakristo wakieleza kuwa hawana pa kukimbilia kwa kuwa ni zaidi ya miezi minne kupita tangu padri Evarist Mushi auwawe kwa risasi, na bado mwenendo wa kesi haueleweki, na kwamba sasa hawajui pa kwenda. (tazama picha za maazishi yake)



Kamanda Mkaadamu amekiri kuwa tindikali ni tatizo, na amesema kuwa wanaendelea kufanya jitihada ili kila kitu kiwe wazi.
                             -Gospel Kitaa-
Padri Joseph Magamba akiwa wodini akipatiwa matibabu

Comments