SABABU KUU 10 KWANINI VIONGOZI WENGI HUSHINDWA KATIKA MAMBO MBALIMBALI (Sehemu ya kwanza)

Pastor Peter Mitimingi.


1.SABABU YA KWANZA
Stadi mbovu za uhusiano na WATU
Kama vile asemavyo John Maxwell mara kwa mara, “Ikiwa watu hawatapatana na wewe, hawawezi kwenda pamoja na wewe.”
Watu ndio rasilimali ya pekee na yadhamani kuliko kitu kingine chochote katika maisha ya uongozi wako.

2.SABABU YA PILI
Mtazamo HASI
Mtazamo wako mwanzoni mwa kazi utayaathiri matokeo ya kazi hiyo kuliko jambo lingine lolote. Hutapanda kufikia viwango vyako kamwe ikiwa utaishi katika shimo la fikra hasi.
Huwezi kuwa na mtazamo mbaya na ukawa na matokeo mazuri.
Mtazamo mbaya, matokeo mabaya pia.
Wewe ukijiona hufai watu wote watakuona haufai.

3.SABABU YA TATU
Kufanya chini ya UWEZO wako
Pamoja na kwamba unalazimika kutathmini mtazamo wako, wakati mwingine unakuwa katika mazingira ambayo hayaendani na uwezo, matakwa, haiba na maadili yako.
Badiliko la kimazingira linaweza kuhitajika ili kukupa nafasi ya kuufanyia kazi uwezo wako.
Unauwezo mkubwa mara nne zaidi ya vile ulivyo sasa endapo utaamua kuupanua huo uwezo ulioko ndani yako sasa.

4.SABABU YA NNE
Kukosa MWELEKEO
Kama Maisha yako hayana mwelekeo, una matatizo – si kwa sababu una shughuli nyingi, bali kwa sababu vipaumbele vyako havijakaa sawa. Hii hupelekea matumizi mabaya ya muda na rasilimali. Hakuna awezaye kupiga hatua ya maendeleo pasipokuwa na mwelekeo.
“Be focused” Huwezi kuwa kila mtu wala huwezi kufanya kila kitu.
Kufanya vitu vidogovidogo vingi, ni sawa na kutofanya kitu hata kimoja.

5.SABABU YA TANO
Hali dhaifu ya KUJITOA (COMMITMENT)
Hali ya kukosa msukumo wa ndani ni ugonjwa wa kufisha katika uongozi.
Hali ya kujitoa ndio dawa.
Vitu vingi vinashindwa kuendelea na kufa kwasababu ya kiwango kidogo cha kujitoa kwa jambo hilo husika.
Mfano, wewe ni mchungaji wa kanisa, lakini hapo hapo una vimiradi vingi vinavyochukua muda wako mwingi. Hatutashangaa kuona kanisa halikuwi miaka nenda rudi.

By Mchungaji Peter Mitimingi.

ITAENDELEA.

Comments