''SALA YA MOYO.

  Na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira

BWANA, Moyoni mwa mtu ndimo ziliko Chemchem za Mawazo Mema na mabaya, tena ndiko kuliko na mauti na Uzima. Kwa kuwa ni WEWE Ndiye Uliyeumba Moyo Wangu hakuna awezaye kuujua Vyema ila WEWE BWANA. NAKUSIHI, Ee BWANA, Peleleza Moyo wangu Uone yaliyomo, na kama kuna Njia iletayo Majuto Ukaniokoe. Wewe MUNGU NDIWE Mwenye haki, Unayevijaribu viuno na mioyo ya watu, Uniondolee kila aina ya Ujinga na Upotofu ndani yangu Nami nitaishi tena. Ondoa Shina la kiburi ndani yangu , ili uovu Ukanitoke mimi, Uutenge Moyo wangu na Kuwaza mabaya na Midomo yangu na Kujipendekeza, nao Ulimi wangu Usinene kwa kiburi.

BWANA, tahiri Moyo wangu, Ondoa Moyo wa Jiwe, Uweke Moyo Msikizi wa Nyama na Uniongoze kwa Haki yako. Sawazisha njia yako mbele ya Uso wangu, wala Usinikemee kwa Hasira yako. BWANA Unifadhili, Uniponye wala Usinirudi kwa ghadhabu yako, bali Uniokoe kwa ajili ya Fadhili zako. Nishike kwa hatamu zako ili nisikutende dhambi, bali nikutolee dhabihu za haki kitandani mwangu. Nakusihi Uniumbie Moyo safi, na ROHO WAKO MTAKATIFU Usiniondolee, maana wewe ndiwe Uwaokoaye Wanyofu wa Moyo. Ee BWANA Nipulizie pumzi yako Fahamuni mwangu, nami nitakuwa Safi tena. Jaza Huruma, Unyenyekevu na Upendo wako ndani ya Moyo wangu BWANA. Uufunike kwa Uaminifu na Utakatifu Wako Nakusihi. Uulinde WEWE Uwezaye Kuulinda ndani ya Damu ya Agano Jipya ya YESU KRISTO, nami nitakuwa Salama. Amina!!!''

Comments