SHOGA MAARUFU DAR AOKOKA, NA KUACHANA NA USHOGA NI ANTI ASU (OTHUMAN HAMIS) SASA ANAITWA AMOSI



Tamaa ya kua na mke na kuitwa baba, ndiyo imemfanya shoga maarufu jijini Dar es Salaam anaye julikana kwa jina la Othuman Hamis au Anti Asu kuamua kuvua gwanda la kua `mototo si riziki’ na kuvaa gwanda jingine la `kidume cha mbegu’. 


Anti Asu ambaye pia ameamua kuokoka na kukiri hadharani kwamba hataurejea kamwe ushoga, inaelezwa kwamba kwa sasa anatafuta mke wa kumzalia watoto na ambaye atampa mapenzi ya dhati.

Imedaiwa kwamba, hivi karibuni Othuman alijisalimisha katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), lililopo Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam ambako alitubu dhambi zake. Sani liliamua kuingia mzigoni kufuatilia `ishu’ hiyo ambapo lilifanikiwa kumnasa Othuman akiwa katika saluni moja ya kike iitwayo Emmy’s iliyopo Magomeni Mapipa jijini anakofanya kazi. Alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kuukana ushoga, kijana huyo alithibitisha ni kweli ameacha tabia hizo na kwa sasa ameokoka baada ya kubadili dini kutoka kwenye uislamu na kwenda kwenye ukristo akiitwa Amos. ``Nimeokoka kiukweli kabisa. Sitaki tena  kuusikia ushoga. Nimemkaribisha mungu katika maisha yangu. Najutia dhambi zangu na namuomba yeye (Mungu) anisimamie na kunilinda ili nisiweze kuanguka tena,’’ alisema Anti Asu ambaye anaonekana ni mwanaume halisi. Amesema kwamba, ameamua kuanza maisha mapya na kwamba anaishi katika kanisa la TAG Magomeni ambako amekuwa akikesha kwa maombi.

``Mimi nilikua shoga namba moja Tanzania baada ya marehemu Anti Kessy. Hakuna alieyekua ananifikia.Nimevunja ndoa zaidi ya 30 na nimetembea na wanaume hata zaidi ya 200. Nimeishi kinyumba na wanaume zaidi ya 10. Nimebwakwa na kufanya kila aina ya ufilauni. Nani ambaye alikua ananifikia mimi?  Shoga gani ajitokeze hapa. Lakini sasa nimeachana na yote haya baada ya kubaini nilikua naitwa na Mungu. Nimeludi kwake na ninahisi amani moyoni mwangu,’’ amesema. 

Ameongeza kwamba kwa sasa anajiandaa kuoa kwani alipima kama ana maambukizi ya maradhi ya Ukimwi na majibu yameonyesha kwamba yupo salama.`` Nashukuru kwamba hata jogoo anawika.’’ Aliongeza kwamba sababu nyingine nyingine iliyosababisha   aokoke ni kutoka na na kuugua sana tangu alipokumbwa na tukio la kubakwa na wanaume zaidi ya 10. Mchungaji Kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Dunstan kanemba amethibitisha kuokoka kwa Anti Asu na kusema kwamba yeye ndiye aliyemuombea na kumkaribisha rasmi kanisani hapo. ``NI kweli Amosi (Anti Asu) tunaye hapa.Ibada ya Jumapili iliyopita tulimuombea hadharani na alidondoka chini. Hii ni ishara kwamba alikua na mapepo yanayomsumbua. Kanisa limempa hifadhi ya kuishi hapawakati tunamjenga kiroho. Pia tunamhudumia kwa mavazi na mahitaji mengine,’’ alisema Kanemba. Aliongeza kwamba uamuzi aliofanya kijana huyo ni wa msingi na kuwataka watu wengine ndani ya jamii wenye matatizo kama hayo kufika kanisani hapo kupata msaada wa maombi. ``kwa yoyote anayehitaji kumsaidia zaidi kimwili basi asisite kufika hapa kanisani. Tunaamini kuwa kuokoka kwake kutasaidia sana kuwafanya vijana wengine wenye tabia hiyo kuokoka pia au kuacha’’ alisema Kanemba.

                                             -Sani-

Comments