UFALME WA MUNGU


Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula

BWABA YESU asifiwe wapendwa.
Nakukaribisha katika somo hili muhimu kuhusu ufalme wa MUNGU.

Ufalme wa MUNGU sawasawa na  ufalme wa mbinguni.
Ufalme wa MUNGU ni miliki/ utawala wa milele na unaanza kabla ya mtu kufa na baada ya kufa.
Neno la kwanza la BWANA YESU alipoanza huduma yake baada ya kubatizwa alisema Marko 1:15 ‘’Akasema, wakati umetimia na UFALME WA MUNGU umekaribia, tubuni na kuiamini injili.’’

UFALME WA MUNGU UTAKUAJE? AU UKO WAPI?


1:   Ufalme wa MUNGU hauji kwa kuchunguza ila ufalme wa MUNGU unakaa ndani ya wateule wa MUNGU.Luka 17:20-21 ( Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa MUNGU utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa MUNGU hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa MUNGU umo ndani yenu.   )

2:   Wengine wamejaliwa kuujua ufalme wa MUNGU na wengine hawajajua.Mathayo 13:11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa. ).
3:    Wengine huupata ufalme wa MUNGU ila shetani huondoa neno la ufalme wa Ufalme wa MUNGU.Mathayo 13:19 (
Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia. )



MFALME WA UFALME WA MUNGU.


-Danieli 7:13-14( Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. )
 
-Ufunuo 11:15 (
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele. )
 

-Isaya 9:6-7( Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo. )
 
-Yohana 8:12(
Basi YESU akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. )
BWANA YESU ndio mfalme wa ufalme wa MUNGU.

JINSI YA KUWA RAIA WA UFALME WA MUNGU.

-Mathayo 7:22 (
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?   )
-Watu wenye dini watagundua siku ya hukumu kuwa hawakuwa sehemu ya ufalme wa MUNGU kwa sababu hawakumpa BWANA YESU maisha yao.
-Wengine wanafanya unajimu na uganga kwa kutumia dini na dhambi nyingine nyingi huku wakidhani matendo yao hayo yatawapa ufalme wa MUNGU kumbe watapata ufalme wa shetani na kama wasipotubu na kumpa BWANA YESU maisha yao hawatakuwa sehemu ya ufalme wa MUNGU .

-       Kuzaliwa mara ya pili Yohana 1:10-13.( Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. )
 
-Wagalatia 3:26 (
Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa MUNGU kwa njia ya imani katika KRISTO YESU. )

 
Ndugu tutumie ufunguo kuingia huko kwenye ufalme wa MUNGU, Kwani unapokua mgonjwa sana, dawa bora kuliko zote haitaweza kukusaidia mpaka utakapoitumia. Na utakunywa dawa pale utakapojitanbua kuwa unaumwa.  Dawa au ufunguo wa kuingia ufalme wa MUNGU ni YESU. Na ukijitambua kuwa unahitaji ufalme wa MUNGU lazima utakunywa dawa ili upone au upokee ufalme.
- Kama una ufunguo wa mlango uliofungwa, mlango huo utabaki umefungwa mpaka utumie ufunguo na utafanya hivyo iwapo unataka hasa kuingia ndani yake, UFUNGUO NDIO YESU KRISTO.
-Mathayo 13:43(
Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie. )


-      - Mathayo 6:33(Bali utafuteni kwanza ufalme waMUNGU, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. )
MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka muda wa kufanya hivyo ni leo, okoka ndugu na uwe raia wa ufalme wa MUNGU.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.

Huduma ya Maisha ya ushindi.

Comments