UJASILIAMALI NA KUJITEGEMEA KWA KIJANA MKRISTO.



Ujasiliamali ni uwezo wa kuitambua fursa na kuitumia.

                              FAIDA ZA UJASILIAMALI
1: Kuishi maisha bila kumtegemea mtu mwingine.( Yaani ajira ya kujiajiri mwenyewe)
2:  Kupata kipato cha kuongoza maisha yako.
3: Miradi ya aina yeyote utakayoihitaji
4: Kutumia karama tulizopewa. Warumi  12:4-8
5: Tujitolee katika nyanja zote iwe ni katika jamii au kwa kazi ya MUNGU.
6:  Kuepuka maisha tegemezi.

                   MATATIZO YANAYOWAKUMBA VIJANA.
A: Uzoefu.
B: Uzembe kazini.
C: Kukosa uaminifu.
D: Ukosefu wa ajira . kuajiriwa au kujiajiri
E: Kuathiriwa na magonjwa. Mfano UKIMWI na TB.
F: Rushwa wakati wa ajira.
G: Elimu duni.
H: Fashion.
     1 Thesalonike 4:1-12 (
Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.  Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;  si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.  Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.  Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.  Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
  Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.
 Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana. Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;
 ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote. )

     KAMA KIJANA NI LAZIMA UTAMBUE MAMBO MATATU(3)

1:  Kujitambua.
Yaani wewe ni nani na wa wapi na nafasi yako ni ipi.
2: Unafanya nini na kwa nini na ili iweje.
Mithali 13:16(
Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu. )
  pia Mithali 24:1(
Usiwahusudu watu waovu, Wala usitamani kuwa pamoja nao;)
3: Kuisaidia familia.
 kifedha, kimawazo, ushauri N.k
4:  Kuisaidia jamii inayokuzunguka
Luka 2:52
MUNGU awabariki sana na ni vizuri kuitambua fursa na kuitumia , huku ukiwa mwaminifu kutoa Fungu la kumi na sadaka kwa MUNGU ili MUNGU ailinde ajira yako hiyo iwe ya kuajiriwa au ya kujiajiri. Pia kama hujaokoka ni wakati muhimu wa kuokoka, maana hata kama utapata yote ya duniani lakini bila uzima wa milele na BWANA YESU ni balaa kuliko zote. MUNGU atusaidie katika hili.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
   Maisha ya ushindi Ministry.

Comments