VITA VYA KUMILIKI * sehemu ya kwanza *

Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Nakusalimu katika jina la Bwana ndugu mpendwa…
Jina la Bwana liinuliwe,Oooh Haleluya…

Ili umiliki ni lazima uwe na nguvu ya tofauti kuwashinda wengine,
Na huwezi kumshinda mtu/falme ikiwa kama hakuna vita.
Hivyo ili ushinde ni lazima vita iwepo.

Palipo na vita ndipo ushindi hupatikana,kwa lugha nyingine ni kwamba ikiwa hakuna vita hakuna ushindi,yeye ashindaye hushinda kwa sababu alikuwepo vitani.

Ipo vita katika kumiliki ipigwanayo katika ulimwengu wa roho,kisha yeye ashindaye huko katika ulimwengu wa roho hudhihilishwa katika ulimwengu wa damu na nyama/ yaani ulimwengu wa mwili.

Sio watu wengi wanafahamu jambo hili,
Lakini kupitia fundisho hili ambalo Roho mtakatifu kaliachilia mahali hapa kwa watu wake ambaye anawataka waishi maisha ya ushindi katika kumiliki yale yote ambayo Yeye Mungu aliyowapa,

na mtu wa namna hii aliyekusudiwa amiliki yawezekana ni wewe mpendwa usomaye ujumbe huu mahali hapa.

Dhumuni kubwa la Bwana Mungu la kumuumba mwanadamu ni KUMILIKI (Mwanzo 1:28),
kwa utukufu wake Yeye,yaani kwa kufanya mapenzi yake tu.Mungu amempa mwanadamu mambo mazuri ya kumiliki,lakini swali la kujiuliza kwa nini basi wengi hushindwa kumiliki ?

*Ipo sababu ya msingi,Bwana akusaidie uweze kuelewa ujumbe huu.

Tazama sasa;
Ikiwa kama mtu anataka kumiliki jambo jema katika ufalme wa Nuru,ujue falme ya giza haitakaa kimya bali itajitahidi kushindana na mtu huyo,ili asije akamiliki na kulitukuza jina la Bwana.
Yeye atakaye kumiliki hana budi kupigana vita. Vita haviepukiki kwa habari ya kumiliki.
Hakuna awezaye kuikemea vita isimpate na ikiwa anataka kumiliki,bali yatupasa kuishinda vita hiyo kwa msaada wa Roho mtakatifu.

Katika dunia ya leo,ili uweze kuishi kwa kumiliki, ni lazima uwe umeegemea katika misingi ya nguvu.

Nikimaanisha kwamba kila mtu umuonaye hivi leo,ipo sehemu ya nguvu ambayo mtu huyo huitegemea katika kufanya kazi,zaidi sana katika kumiliki.

Zipo nguvu za aina mbili tu hapa ulimwenguni;
Yaani
*nguvu za giza/falme ya giza.
*Nguvu ya Nuru/falme ya Mungu mwenyewe.

Hivyo yeye amilikiaye naye huitaji nguvu ili aweze kumiliki.Pasipo nguvu hakuna kumiliki kwa namna yoyote ile.

Yapo mambo yatupasayo kufanya,ambayo yanatupa ushindi katika vita vya kumiliki ambayo vita hiyo kiukweli kabisa Bwana ni lazima hausike ili tuwe na ushindi,tena ushindi dhidi ya dhambi.

Jambo la kwanza ni;
01.Hakikisha mausiano yako na Mungu yako sawa

Kumb. 1 :42
“ Bwana akaniambia, Uwaambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi si kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu.”

Bwana anajaribu kufikisha ujumbe kwa wana wa Israeli kwamba wao wenyewe hawana huwezo wowote wa kwenda kumiliki katika nchi ambayo Bwana alikuwa amewahaidia pasipo Yeye Bwana kuwa kati yao.

Kumbuka hili;
*Wana wa Israeli walihaidiwa kupewa nchi mpya,(Kanaani)lakini wengi hawakufika huko ingawa walihaidiwa.
Walikuwa katika ugeni,mahali ambapo sio mpango wa Mungu kukaa hapo daima,
Hivyo walihitajika watoke na kwenda kwa kufuata kusudi la Mungu ili waende kumiliki ,
Katika kutoka kwao kwenda kumiliki yote aliyowapa Bwana Mungu ,ilikuwa ni vita kali maana wengi walikufa njiani .

-Mfano wake ni kama leo hii sisi wapendwa tunavyoelekea Kanaani.Katika safari hii ya kuelekea kwenye nchi mpya(mbingu) wengine hawatafika ingawa wapo safari moja ya watu waelekeao huko.

Hapo sasa Bwana anatutahadhalisha kwamba tusiende kupigana ikiwa Bwana hayuko upande wetu,kwa lugha nyingine ni kwamba Bwana anatuambia hatutaweza kushinda vita ya kumiliki pasipo mkono wake.

Oooh kumbe!
Ndipo sa nimegundua kwamba mkono wa Bwana una UTIISHO pindi tuwapo vitani kwa habari ya kumiliki…

ITAENDELEA…

*Tafadhali usikose muendelezo wa fundisho hili mahali hapa.
Kwa maombezi na kujuliana hali,mawasiliano ni
0655-111149,
0783-327375

UBARIKIWE.

Comments