VITA VYA KUMILIKI * sehemu ya pili *

na Mtumishi wa MUNGU, Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiwe…
Nakusalimu katika jina la Bwana ndugu mpendwa…
Jina la Bwana liinuliwe,..
Haleluya…

Nilikuambia kwamba ipo vita katika kumiliki,
kwa maana ni hivi,ni kweli umepewa umiliki lakini hapo hapo ufalme wa giza hawezi kukaa kimya wakati wa kumiliki kwako kwa kitu chochote kile.

Ni napozungumzia habari ya kumiliki sizungumzii kumiliki Nyumba au mapesa fulani au magari tu,HAPANA HIVYO VYOTE HAVITOSHELEZI NENO “ KUMILIKI”

Bali kumiliki ninakokuzungumzia ni juu ya mambo yote tuliyopewa yawe chini yetu,tuyatawale.
Maana Mungu alitumilikisha URITHI wake, tukatawale vitu vyote na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Hivyo utagundua kwamba tumepewa KUMILIKI vitu/Mambo yote yaliyo hai.( Mwanzo 1:28)

Hivyo tena ukimuona mtu anamiliki kitu kilichokufa basi ujue bado hajamiliki,au hajawahi kumiliki kabisa maana tumepewa kumiliki vilivyo hai.

Katika ulimwengu huu kamwe hatuwezi kumiliki ki-urahisi rahisi tu maana ipo vita katika kumiliki.
Tazama Mungu amwambiavyo Yoshua mtu wake,
“ Uwe hodari na moyo wa ushujaa,
maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. ” Yoshua 1:6.

Ingawa Mungu alikuwa upande wa kina Yoshua lakini bado akimsisitiza kwamba yampasa Yoshua awe na moyo wa USHUJAA sababu kitendo cha kuwalisisha Waisraeli katika nchi aliyowahaidia Bwana ni lazima vita ipiganwe,ndiposa waweze kumiliki.

Kama vile sisi tulivyohaidiwa mbingu mpya na nchi mpya baada tu ya maisha haya kupita,hapo sasa ni lazima tupigane vita vizuri ili tuweze kumiliki nchi hiyo atupayo Bwana Mungu.

Sisi wana wa Mungu tumepewa kumiliki,lakini cha kushangaza tumeshindwa kumiliki,
yaani hata baadhi ya mambo makubwa yamemilikiwa na watu wa mataifa hali nasi tupo,
Hii inatupatia picha kwamba hatujapigana vita vyakutosha.

Ngoja nikupe mfano kidogo hapa, tazama watumishi wa Mungu wote walioandikwa katika Biblia walikuwa na nguvu ya kumiliki,
na ukweli ni kwamba walimiliki yale mambo makubwa katika nchi husika,
tukianza hata kumuangalia Ibrahimu,na wengine.

Utagundua kwamba walikuwa na utiisho wa nguvu ya kumiliki nadni yao,mtizame Ibrahimu yeye alimiliki mifugo mingi mno hata kukakosa inchi/ardhi ya kuwaifadhi mifugo hiyo pindi ndugu yake Lutu alipokuwa na mifugo mingi tena
Maandiko yanatuambia mpaka kukawapo ugomvi kwa wachunga wanyama wa Lutu na wachunga wanyama wa Ibrahimu;

Mwanzo 13:6-7 ;
“ Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja.
Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi.”
-Na mambo mengi tu aliyokuwa nayo.

Sasa watu wa leo mimi nawashangaa kabisa maana wanafahamu kuwa umeokoka ni kuwa na maisha duni,
yaani mlokole akiwa na nguvu ya kumiliki mali basi hapo utaona maneno atakayorushiwa na walokole wengine,
wengine utawasikia wakiwasema watumishi vibaya wakidhani kwamba imetupasa kuishi kimaskini,

*Mungu awasaidie watu wa namna hii kwamba ufahamu wao ukombolewe katika jina la Yesu Kristo.

Jambo moja nililokuambia katika sehemu iliyopita ikiwa ni mojawapo ya sababu ya msingi ya kushinda vita hivyo vya kumiliki nilikuambia kwamba;

01.HAKIKISHA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU YAKO SAWA.

Hakuna awezaye kuishinda vita ya kumiliki pasipo msaada wa Mungu,kwa maana ikiwa tutaenenda kwa akili zetu binafsi basi ni dhahili kabisa twataka kufa.
Lakini kwa msaada wa Mungu kila kitu kinawezekana.
Ninapokuambia kwamba mahusiano na Mungu wako yawe sawa,
ninazungumzia kwa habari ya kuwa rafiki wa Mungu.

Maana yeye mwenye urafiki ndio mwenye mahusiano mazuri,kwa lugha nyingine huwezi kuwa na Mahusiano mazuri kwa yeye ambaye si rafiki yako…

ITAENDELEA…

*Tafadhali usikose muendelezo wa fundisho hili mahali hapa.
Kwa maombezi na kusalimiana mawasiliano yangu ni
0655-111149,
0783-327375

Comments