WEWE NI MWANA AU MTOTO, AU NI MSHIRIKA AU MKRISTO TU?




Na Bishop YONA   P  SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
karibu kwa maombezi na ushauri wa kibiblia



  -Lugha ya Mwana  ina uzito kuliko lugha ya mtoto.
   Wote waliompokea Yesu walifanyika wana wa Mungu. (Yh 1: 12)
Mwana hufanywa, unaweza kuzaa mtoto asifanyike kwako mwana akabaki kuwa mtoto.  
 -  Mwana anapaswa kumpokea Baba moyoni na Baba ampokea mwana moyoni.  
 - Kinachomfanya mwana ni mwonekano wake mbele ya Baba yake( kwa utii, unyenyekevu, usikivu, kujitoa kwa Baba yako Mf. Priska, akila Rum 16: 3-4)  
-   Mwana siku zote akiwa mbele za Baba yake kumsikiliza anachotakiwa kufanya ( Yoh 5:19 mwana hutenda kile Baba anachotenda)  
 - Ili uwe mwana lazima uwe na Baba atakayekufanya huo uwana.
 -   Baba yako ni nani? Au una wababa wangapi wa kiroho? ( Filipo tuonyeshe Baba Yoh 14: 6-13)
 -   Uhusiano wako na Baba yako ukoje? Ushirikiano wako na Baba ukoje? (Mal 1:6a)
 -   Mwana hufanya mapenzi ya Baba (Yoh 4:34)
 -  Mwana atafuta wazo la Baba ni lipi ili alifanye pia humtukuza Baba (Yoh 17: 3-6a).
  -  Mwana afanya kile Baba anachokifanya, mnaniita Bwana Bwana na hamfanyi niyatendayo.
 -  Mwana hawezi kujitukuza au kujibariki mwenyewe ( Math 3:16-17, Luka 9:33-35)
 -   Ule uzima Baba alionao na mwana anakuwa nao mara dufu (Yoh 5:26).
  - Huwezi ukawa na Baba wengi, Baba ni mmoja kubali kukaa chini ya Baba ili uwe baraka (1Kor 14:17)


MUSA NA MWANAYE WA KIROHO:

-   Musa na wana wa Israel, Wana wa Israel hawakukubali kuwa wana wa Musa matokeo walikufa wengi.
Mungu alimwinua Musa awe Baba kwa wana wa Israel.
Musa aliambulia watoto wawili Joshua na Kalebu.
- Wana wa Israel walikuwa mzigo (Mith 19: 13).
- Paulo na Timotheo mwanaye.
- Paulo alikuwa Baba wa Timotheo.
-Timotheo alifanywa mwana na Paulo.

MAMBO YANAYOMFANYA TIMOTHEO AWE MWANA WA PAULO:
-Alikubali kukaa chini na kulelewa na Paulo (1Tim 1:1-3)
 -Alikubali kubeba agizo la baba yake
- Alikubali kuelekezwakupokea maagizo (Tim 1:18-20, 2Tim 3:10)
 -Timotheo alikuwa mwana kwa baba Paulo (1Tim 4:16)
- Timotheo alimwombea baba yake, aliufurahisha moyo wake (2Tim 1:2-8 hakuona kuitwa baba yake).
- Mwana ni faraja kwa babaye (2Kor 7: 5-7)
 -Mwana hufanywa (shika kielelezo maneno ya uzima uliyosikia kwangu (2Tim 1: 13-14).
 -Timotheo alimwepuka baba yake mst 15 (2Tim 4:9,13)_
- Onesiforo aliuburudisha moyo wa baba yake mst 16.
- Ili mwana awe baba kwa wana anapaswa akae kwenye mafundisho ya baba mmoja, 2Tim 3: 14 – 17.
 -Ni vizuri unyonye maziwa kwa mama mmoja.
 -1Petro 2:2 unanyonya maziwa wapi na wapi ( Tamani kunyonya maziwa sehemu moja).

-Mkristo anapoondoka kwenda sehemu nyingine anaitwa mtoto (mwana anaishi, anakaa, anaishi karibu anatumika kwa wakati huu) Filemoni 1: 10-13.

- Huyu alikuwa moyo wa Paulo Onesmo
 -Paulo alimkabidhi mtoto akawa mwana kwa Filimoni (ubaba ulivyo akiwa anadaiwa kitu nidai mimi mst 17 -21)
 -Kadri mwana anavyokuwa karibu na baba ndivyo baba anavyoachilia heshima kwa mwana (Yoh 5: 22-23 mwana yupo tayari kujitolea maisha yake kwa ajili ya baba amlinde Mf, Priska, Akila (Rum 16: 3-4)

- Yale maisha ya Yesu mbele ya baba yake na yale maisha ya Timotheo mbele ya baba yake Paulo,na Elia na Elisha na Musa na Joshua ndivyo Mkristo mwenye kuhitaji kuwa na mafanikio endelevu anatakiwa aishi mbele ya Mchungaji wake.
MUNGU akubariki sana
 by Bishop YONA   P  SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
karibu kwa maombezi na ushauri wa kibiblia

Comments