ALIYEKUWA BUBU NA KUSHINDWA KULA MWENYEWE AFUNGULIWA BAADA YA MAOMBEZI


Kijana Betheli akiongea vizuri mara baada ya maombezi
Siku ya 12 ya mkutano wa Mch. Josephat Gwajima ambaye ni Askofu wa kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church maarufu kama Ufufuo na Uzima, imekuwa siku ya miujiza mingi, kuna na matendo makuu ambayo Mungu ameyafanya katika viwanja vya Angle Shellaton jijini Arusha mojawapo likiwa la kijana aitwaye Betheli aliyekuwa bubu asiyeweza kuzungumza kwa miaka mingi; kuponywa ububu wake baada ya maombezi kutoka kwa Mch. Gwajima.



Akiongea kwa furaha na huku akimtukuza Mungu mama yake mzazi aitwaye Grace alisema, mbali na ububu uliokuwa ukimsumbua mwanaye; pia alisumbuliwa na magonjwa mbalimbali kiasi kwamba alikuwa hawezi kula chakula mwenyewe maana alikuwa ni mtu wa kulazwa kitandani tu kwa muda wa miaka mitatu bila msaada wowote.

Mama mzazi wa Betheli akielezea tabu aliyoipata
juu ya mwanaye
Ili kudhihirisha kuwa anaweza kuongea mwenyewe Mch. Gwajima alimwambia ataje maneno ambayo kwa hapo awali hakuweza kutamka kabisa; Kijana Betheli aliongea vizuri akiwa ameponywa kabisa kwa kuyatamka kama yalivyo. Baadaye Mchungaji akaamuru apewe maji naye aliweza kunywa mwenyewe jambo ambalo hakuweza kulifanya kwa miaka mingi sana.

Kuelezea ushuhuda huo, mama yake alisema kuwa alisafiri na mwanaye kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro kuja Arusha kwaajili ya kuhudhuria kwenye mkutano huo. Mama huyo ambye alijawa na furaha sana baada ya kushuhudia mwanye akiongea mwenyewe alisema kuwa anamshukuru Yesu Kristo sana kwa uponyaji wa mwanaye.

Alisema, miaka mitatu ya magonjwa yake alisumbuka naye sana kila mahali bila mafanikio lakini ana mshukuru Yesu kwa kumweka huru mwanaye anasema hana la kumpa bali ni kumsifu na kumshukuru Yesu Kristo.
Kijana Betheli akinywa maji mwenyewe baada ya kuponywa yaliyokuwa yakimsibu
MUNGU KWETU SISI NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE!!!

Comments