APONYWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA MWANAUME WA ROHONI


Suzana Temba
Suzana Temba alikuja mkutanoni siku ya sita akiwa amekata tamaa ya maisha kutokana na matatizo mengi ambayo yalikuwa yanamzonga katika maisha yake. Suzana ambaye ni mkazi wa Arusha alipata taarifa za mkutano na kuamua kuja akiamini kuwa Mungu atamponya.



Kuhusu ushuhuda wake, Suzana alikuwa na haya ya kusema, "nilipofika ibadani nilishangaa kuona kila neno ambalo Mchungaji Gwajima alikuwa akifundisha lilinihusu mimi" Aliendelea kusema kuwa wakati wa maombezi ulipofika alisogea mbele na hapo akapokea uponyaji wake kamili.
Suzana Temba akihojiwa na mwandishi wetu mara baada ya maombezi
Akihojiwa na mwandishi wetu, Suzana alisema kuwa familia yao kwa miaka mingi ilikuwa katika matatizo ya vifo vya hovyo hovyo ya kwamba misiba ilikuwa haiishi katika familia yao. Jambo linalotia shaka ni kwamba vifo vingi ni vya kufanana mfano kifo ambacho baba yake alikufa kinafanana kabisa na namna ambayo mdogo wake alikufa.
Suzana akiwa na furaha baada ya kufunguliwa na kuwekwa huru kabisa
Tatizo lingine lililomsumbua na kumfanya akose raha ni maumivu ya kiunoni ambayo kwa miaka mingi alikuwa anasikia kama moto unawaka kiunoni mwake. Pamoja na maumivu ya kiuno Suzana aalikuwa anatapika mara kwa mara bila kuelewa chanzo na kwa maelezo yake hospitali nyingi hazikuweza kutmtibu moja kwa moja.

Pamoja na hayo yote, Suzana alikuwa anasumbuliwa na mume wa rohoni maarufu kama jini mahaba; ambaye alikuwa anamsumbua wakati wa usiku hadi kufikia hali ya kutokuwa na hamu na mumewe kabisa jambo lililopelekea kuachana na mumewe. 

Baada ya maombezi, Suzana akawekwa huru kabisa na sasa hamuoni tena yule mume wa rohoni na pia anasikia tumaini jipya na amani moyoni mwake. ASANTE YESU KWA KUNIPONYA

Comments