ASKOFU KAKOBE ANAWASHA MOTO WA INJILI KONGO

Askofu Kakobe akiwaombea wachungaji katika semina mjini Lubumbashi jana.
Baada ya mkutano mkubwa wenye mafanikio alioufanya jijini Toronto nchini Canada mapema mwezi wa sita mwaka huu, Askofu Zachary Kakobe amerejea tena mjini Lubumbashi nchini Kongo ambako anafanya mkutano mkubwa wa injili uliopewa jina la "Great Miracle Healing Crusade" ambao umeanza jana ijumaa tarehe 18/10/2013 na utamalizika hapo kesho siku ya jumapili.

Kabla ya kuanza mkutano huo ambao umekusanya maelfu ya wakazi wa jiji la Lubumbashi, askofu Kakobe alianza na semina maalumu kwa wachungaji wa makanisa mbalimbali ya kiroho nchini humo iliyofanyika kwa siku mbili Alhamis na jana ijumaa ambapo pia alipata kuwaombea ujazo wa Roho Mtakatifu wachungaji hao ambao kwa mujibu wa taarifa kutoka huduma ya askofu Kakobe wachungaji hao wameshukuru kwakujazwa nguvu mpya katika kuitenda kazi ya Mungu katika makanisa yao.


Kundi la wachungaji waliohudhuria semina hiyo.


Picha mbalimbali zikionyesha semina ya wachungaji ilivyofanyika huko Kongo Alhamis na jana Ijumaa. Picha kwahisani ya ukurasa wa Facebook wa huduma ya askofu Kakobe.

Comments