BAADA YA MUNGU KUJIDHIHIRISHA KILIMANJARO, UFUFUO WAPATA JENGO MAELFU WAHAMIA


Jengo linavyoonekana kwa nje.

Baada ya kumalizika kwa mkutano mkubwa wa injili viwanja vya mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, mmoja kati ya watu waliohudhuria katika mkutano huo ametoa jengo lake kubwa ili litumiwe na kanisa la Ufufuo na uzima kwaajili ya huduma mbalimbali zikiwemo ibada.

Kitendo cha kanisa hilo chini ya mchungaji wake kiongozi Josephat Gwajima kilitarajiwa na wengi hasa kutokana na mafundisho yaliyofundishwa na mchungaji huyo pamoja na watu kuwa sehemu ya miujiza iliyokuwa ikitokea katika uwanja wa mashujaa hata ilivyokuwa mkoani Arusha.

Tayari kanisa hilo limeshaanza mafundisho ya neno la Mungu kwa maelfu ya watu wanaohudhuria katika kanisa hilo jipya baada ya kulifanyia usafi wa hali ya juu ulioongozwa nguvu na mama Grace Gwajima, kutokana na vumbi iliyokuwa imelifunika jumba hilo. Mahudhurio ya watu katika mkutano wa Arusha na Kilimanjaro yamevunja rekodi ya kuhudhuriwa na watu wengi sana kuzidi hata mikutano yenye wahubiri kutoka nje ya nchi.

Kanisa hilo kwasasa linajiandaa na mkutano mwingine mkubwa utakaofanyika mwezi ujao mkoani Tanga, kabla ya kuelekea mikoa mingine ikiwemo Kigoma, Iringa na Morogoro.




Watu wakiwa wamejaa tayari kwa kusikia neno.

Muziki ukiwa uko sawa na watu wako tayari.

Sehemu ya umati wa watu waliojaa katika jengo hilo.

Comments