JE! HAYA NDIYO MAAGIZO YA KRISTO?



Wakristo wengi wamekuwa na tabia ya kuhubiri madhehebu yao na huduma zao na wamesahau kumhubiri YESU KRISTO MUNGU ALIYE HAI je! haya ndiyo maagizo ya Kristo? Yesu aliagiza kwa wanafunzi wake kuwa ''' Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe aaminiye na kubatizwa ataokoka''' sasa inakuwaje leo tunahubiri madhehebu? utasikia njoo huku ndio kwenye njia ya kweli, mara uponyaji unapatikana hapa tu, wengine MUNGU wa kweli anapatikana hapa tu, tena mwingine utasikia fika kwenye kanisa letu au huduma yangu ndipo kuna uponyaji wako, yaani kama mimi nipo Zanzbar nipande boti nije hadi Dar ili kutafuta uzima, hata Mungu anatushanga yeye anapatikana popote kwa imani tu, tuache unafiki, yaani mimi pamoja na wewe, uponyaji na uzima unapatikana kwa Yesu pekee na yeye ndiye njia ya kweli na uzima, wengine wanaacha kuwahubiri machangudoa walevi majambazi na waliopotea kwa ujumla kazi kuwashawishi walokole wahamie kwenye madhehebu yao, hiyo ni injili feki tena huo ni ushetani .
ushauri wangu tuhubiri habari za toba msamaha na ondoleo la dhambi kupitia kwa YESU KRISTO kwani mbinguni hakuna madhehebu wala dini ni watakatifu tu ndio watakao ingia. TUJIREKEBISHE

MUNGU awabariki sana
By Baraka Mhunda Zanzibar Pentecostal Church.(P A G)  Chukwani.
.

 

Comments