Maelfu ya wakazi wa Geita na viunga vyake
walikusanyika nyumbani kwa mzazi wa shabani maulidi lilipo kaburi hilo
kushuhudia ufukuaji wa viungo vya mtu anayedaiwa kufariki na kuzikwa,
ambapo mtaalam wa maabara ofisi ya mkemia mkuu kanda ya ziwa Bwana Lucas
Nduguru amesema kazi ya kuchunguza vipimo vya vinasaba (DNA) vya
kijana huyo pamoja na wazazi wake, itakamilika ndani ya wiki mbili hadi
mwezi mmoja ili kuthibitisha ukweli wa kupatikana kwa mtu
aliyekwishafariki akiwa hai.
Baadhi ya wananchi wamesema wameshangazwa na tukio hilo na kuiomba serikali kutoa majibu sahihi ili kujua ukweli wa jambo hilo.
kijana Shabani Maulidi anadaiwa kuwa alifariki
mwaka 2011 na kuzikwa nyumbani kwao, cha ajabu tarehe 28 mwezi wa nane
mwaka huu mama yake mzazi alimkuta katika majaruba ya mpunga akiwa hai
na mpaka sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya
Geita.
video ni hii hapa
chanzo: ITV
![]() |
Comments