KANISA LA T.A.G KUANZISHA BENKI

Askofu Barnabas Mtokambali wa T.A.G



KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) lipo katika mchakato wa kuzungumza na wasomi ili kuanzisha benki yao.

Hayo yalielezwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Barnabas Mtokambali, wakati akizindua jengo jipya la Kituo cha Uamsho na Umisheni lililopo Msasani.

Mtokambali alisema haiwezekani wakakosa wasomi wenye mioyo ya kusaidia kanisa hilo kuanzisha benki, hospitali na chuo kikuu.

“Sisi tuna uwezo wa kuanzisha chuo kikuu kupita hata kile cha Dodoma na hospitali kupita ile ya KCMC na jambo hili linawezekana kabisa kama kutakuwa na lengo na nia katika hilo,” alisema Mtokambali.

Askofu huyo alisema si vema nyumba za ibada kutumika kwa kufanya biashara na mambo ya siasa.

Mchungaji wa kanisa hilo Mashariki Kaskazini, Samson Swila, alisema jengo hilo limegharimu sh milioni 146 hadi kukamilika kwake, na kuongeza kuwa wamekabiliana na vikwazo vingi lakini Mungu aliwasimamia.

Source : Tanzania Daima.

Comments