KUDUMU KATIKA MAOMBI

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Namshukuru Mungu kwaajili yako unaesoma ujembe huu-Mungu akubariki sana na kukuepusha na balaa zote,afute laana na mikosi inayokuzunguka katika jina la Yesu Kristo.

Ndugu yangu, naomba nikukaribishe katika somo letu la leo:

MADA KUU: KUDUMU KATIKA MAOMBI.

Kwanza Kabisa,naomba kukueleza kwaufupi sana kuwa Dhana ya "kuomba" ni kuwasilisha mahitaji ili upatiwe msaada.
Aidha, kwa muktadha huu, kuomba ni kuwasiliana na Mungu ambaye ndiye baba yetu na mwokozi wa maisha yetu-Haleluya!

(A)Maandalizi kabla ya kuanza Kuomba.

(i) Hakikisha Moyo wako ni safi mbele za Mungu, usiwe na kinyongo,hasira wala mwenye mawazo mabaya, hivyo jitakase kwanza kabla ya kuanza maombi.Zaburi 29:2b...mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu
(ii) Tubu ili utakaswe hata Mungu akusikilize,omba rehema za Mungu ziwe juu yako ndipo uanze kuomba Isaya 1:18.

(B)Namna ya kuomba.

(i) Kwanza maombi ni lazima ujue unaomba nini na kwa nani.
Yesu alisema, na lolote mtakaloomba kwa Baba yangu, ombeni kwa jina Langu,tena akasema, na lolote mtakaloomba kwa jina langu, mmeshapata.
Hivyo, yakupasa kuomba kwa usahihi,kupitia Jina la Yesu kwa kuwa ndilo jina pekee tulilopewa wanadamu kuolewa kwalo....na zaidi hili ndilo jina kuu kuliko majina yote Wafilipi 2:10-11
Maana yake ni kuwa,kuomba kwa kupitia jina lingine ni sawa na kukosea namba za unaempigia simu,je unataegemea kumpata unayempigia simu?
Kwa ufupi. usalipo usizunguke,piga moja kwa moja kwa Yesu naye atatenda hapo hapo.
(ii) Jenga Imani ya kuwa Mungu hashindwi wala si kigeugeu,kila uombacho sharti upate kwa mapenzi yake. Mathayo 7:7,tena kuwa thabiti katika maombi yako hata kwa kufunga Mathayo 17:20-21.
(iii) Kuwa na msatari wa kusimamia katika maombi yako,kwa kuwa Bwana anasema leteni hoja zenye nguvu, tena anaongeza "unikumbushe na tuhojiane....Isaya 43:26,BWANA anakuona na yuko tayari kukuhudumia endapo utachukua hatua ya kuomba kwa imani Yeremia 29:11-12
(iv) Kuwa tayari kwa matokeo yoyote ilimradi yameamriwa na Mungu yatokee,Shukuruni kwa kila jambo,na kila jambo na wakati wake,usilazimishe Mungu afanye vile unataka,yaache yaliyomapenzi yake yatimie Mathayo 7:10,pia Muhubiri 3:1.

(C)Mwisho wa Maombi.
Hitimisha kwa kushangilia kwa kuwa Mungu ameyasikia maombi yako na yuko tayari kufanya vile anavyoona inafaa.

Jitakase tena,omba ulinzi wa Roho mtakatifu,soma biblia,endelea kukua katika hali ya kumpenda Mungu na Utamani zaidi kujifunza mengi kutoka kwake.Mungu akubariki,akuinue na ukupe muujiza wake katika jina la Yesu Kristo.

Amen

 Kama unahitaji kuokoka, au ungependa kupata ushauri wowote maombezi au kutoa ushuhuda, wasiliana na

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7 (57/84) 464 141/ 12 909 021.
Au Email sos.sesi@yahoo.com / newelshaddai@gmail.com
Tunakushauri, utembelee kanisa la kiroho lililo jirani yako, kwaajili ya mafundisho zaidi na Ushirika. (Kumbukumbu la Torati 28:6).

Comments