"KUFANYA AGANO JIPYA NA MUNGU"

Na Abel Suleiman Shiriwa

Unapoamua kuokoka, na kumfuata Mungu, basi unapaswa kujua kuwa, ni Lazima pawe na Agano katika yako na Mungu.
2 Wafalme 23:3 Mfalme akasimama karibu na nguzo, akafanya agano mbele za BWANA, kumfuata BWANA, na kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, na amri zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kuyathibitisha maneno ya agano hilo yaliyoandikwa katika Kitabu hicho; nao watu wote wakalikubali Agano lile.
AGANO NI NINI?
Agano ni makubaliano ya Pande mbili tofauti..
Hivyo katika Agano huwa kuna Masharti ambayo yanatakiwa kufuatwa..
Hivyo unapoamua kumtumikia Mungu, ni lazima ukubaliane na Masharti ambayo Mungu anayataka uyafanye katika Agano hilo, hapa nitaeleza Machache.
1. KUSHIKA AMRI ZA MUNGU.
Ezekieli 20:11 Nikawapa amri zangu, na kuwaonyesha hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo.
EZEKIELI 20:19 Mimi ni BWANA, Mungu wenu; enendeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu na kuzitenda.
2. KUWA MTAKATIFU.
Walawi 11:44 Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.
3. UNYENYEKEVU.
5:5 vivyo hivyo ninyi vijana, Watiini wazee. Naan, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
3. UTII
Warumi 16:19 Maana Utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.
5. UAMINIFU.


2 Wafalme 22:7 Lakini hawakuulizwa habari za ile fedha waliyokabidhiwa; maana walitenda kazi kwa uaminifu.
HIVYO UNAVYOYAFUATA MASHARTI YA AGANO LAKO NA MUNGU, BASI TARAJIA KUPATA MEMA, NA AHADI YA MUNGU, YA KUKUPATIA UZIMA WA MILELE. (Waebrania 10:36-38)
Na ukienda kinyume na Masharti ya Mungu katika Agano lake, tarajia Kupata Mateso ya Milele katika Moto wa Jahanamu, (Ufunuo 21:8)
HIVYO YATUPASA KUDUMU KATIKA AGANO LETU NA MUNGU, ILI TUVUNE MEMA.

Comments