KUJIHESABIA HAKI HULETA KIBURI


Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula, Maisha ya ushindi Ministry

Ndugu BWANA YESU asifiwe.
Nakukaribisha katika somo hili ambalo ni chanzo cha machafuko makanisani na kwenye jumuia za au vikundi katika kanisa, pia jambo hili linaweza kuwa ni chanzo cha mtu kutokubarikiwa. Biblia inasema

{Yakobo 4:1-6 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?  Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?  Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. }

MUNGU huwapinga  wajikuzao  na  huwapa  neema  wanyenyekevu

-Neno  wajikuzao =kiburi 

Ikiwa  mtu  yuko  na  kiburi 

1- kiburi  ni  kikwazo  cha  makusudi  ya  MUNGU {Ayubu  35:12Hulia huko, lakini hapana ajibuye, Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu. }   


2- Kiburi  ni  kikwazo cha  uamsho {zaburi 12:3 Bwana ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi; } 

3- Kiburi  ni  kikwazo  cha  umoja {mithali 8:13Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. }

4- Kiburi  ni  kikwazo  kwa  kuwafikia  wanajamii ambao wanaihitaji kweli ya MUNGU {mithali 13 :10Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana. }

5- Kiburi  huzuia  neema  ya  MUNGU  ndani  ya  kanisa

   na pia BIBLIA inasema
{mithali 15:25 Bwana ataing'oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane. }  PIA {mithali 16:5-8Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu.  Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.  Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. }


                          DALILI   ZA  KIBURI


1-   Kiburi  ni  kukufanya maalumu  na  wakipeeke

Mfano  dhehebu,rangi,elimu,ujuzi

2- Kiburi hutuelekeza  kwenye  roho  ya  kuhukumu

Mfano  dhehebu,rangi,elimu,ujuzu

3- Kiburi  hutufanya   kuangalia  yale  tusiyo  yaona  na  badala  ya yale tunayoyaona

Mfano  sijafanyiwa jambo  fulani ambalo nilitakiwa kufanyiwa

4- Kiburi  huleta wivu

-Unapo barikiwa unasema  ningepata  na  kile

-kwanii  abarikiwe mwingine  na  si mimi

5-  Kiburi  kinatufanya tuwaze  watu  wengine  wananifikiliaje  na  si  MUNGU 

6-  Kiburi  hutufanya  tusiguse utukufu wa  MUNGU –sifa ,heshima,unataka upewe wewe  na si MUNGU

7-Kiburi humfanya  mtu kuwa  na  roho  ya kiburi 

Kiburi  kinatabia  ya kujihami na kujitetea .   
MUNGU akubariki sana na siku zote neno la MUNGU linatutaka tutengeneze kwa ile sehemu tuliyoanguka, kazi ni kwako ndugu tukumbuke kuwa MUNGU huwapinga wenye kiburi.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula
                   Maisha ya ushindi Ministry

Comments